Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Kamanda Mohamed Mpinga.
…………………………………………………………………
Na Mobini Sarya, Tanpress
JESHI la Polisi nchini
kwa kushirikiana na Mamlaka mapato nchini (TRA) limeboresha mfumo wa
utoaji leseni za udereva ambazo zimeanza kutolewa kwa njia aya Smart
Card ili kuendana na ukuaji wa Teknolojia duniani.
Wakizungumza na wandishi wa
habari jijini Dar es Salaam, Mnadhimu wa kikosi cha usalama barabarani
ACP Johandani Kahatano na Naibu Kamishna wa TRA Yusuph Salum wamesema
kuwa mwisho wa kubadilisha leseni kwa maedeleva wote ni Machi 31 Mwaka
huu.
Wameeleza kuwa baada ya muda huo
zoezi la ubadilishaji Leseni za aina zote halitafanyika na mfumo wa
utoaji Leseni utabadilishwa ili kubakia na uwezo wa kutoa Lesseni kwa
madereva wanaoomba Lesseni kwa mara ya kwanza.
Hivyo madereva wote wametakiwa
kuhakikisha wanatumia muda huo wa miezi mitatu iliyotolewa kubadilisha
Leseni zao ili kujiepusha na usumbufu unaoweza kuwapata.
Aidha Kamanda Kahatano amesema
kuwa Dereva atakayekutwa anaendesha gari wakati leseni yake imekwisha
atafikishwa mahakamani pamoja na mmiliki wa gari hilo.
Zoezi la kutoa leseni mpya
za udereva lilianza Oktoba Mosi Mwaka 2010 kwa awamu ya kwanza
iliyohusisha mikoa (9) na machi 2011 mikoa mingine 13 ilianza kutoa
leseni hivyo zoezi hilo kukamilika.
Kamanda huyo amesema kuwa
madhumini ya zoezi hilo ni kubadili mfumo huo na kuondoa tatizo la
kughushi pamoja na kudhibiti mienendo ya madreva kwa kutunza
kumbukumbuku za makosa yao.
Hadi kufikia Disemba 31 Mwaka
jana leseni 616,349 zilizokuwa zimetolewa kwa nchi nzima ambapo kati ya
hizo leseni 135721 ni za kundi lenye madaraja C zingine 480,628 ni za
makundi mengine.
Hata hivyo takwimu hizo
zikilinganishwa na idadi ya vyombo vya moto vilivyosajiliwa na Mamlaka
ya TRA nchini hadi kufikia Disemba 2012 vinafikia 1,164,574 hiyo
inaoonyesha kuwa kuna madereva wanaoendesha vyombo vya moto bila ya kuwa
na leseni halali.
No comments:
Post a Comment