Rais
wa Zanzibar Dk Ali Mohd Shein akikata Utepe kuonyesha Ufunguzi wa Kituo
Kikuu cha Kurushia Matangazo ya Dijitall huko Rahaleo Mkoa wa Mjini
Unguja.ikiwa ni Shmra shamra za Kuadhimisha Sherehe za Kutimia Miaka 49
ya Mapinduzi ya Zanzibar.
PICHA NA YUSSUF SIMAI -MAELEZO ZANZIBAR.
Kituo
kikuu cha Mtambo wa Kurushia Matangazo ya Dijitall kilichofunguliwa na
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza La Mapinduzi huko Rahaleo Mkoa
wa Mjini Unguja.ikiwa ni Shmra shamra za Kuadhimisha Sherehe za Kutimia
Miaka 49 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Rais
wa Zanzibar Dk Ali Mohd Shein wapili kushoto akipata maelezo mafupi kwa
Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Agape Association LTD Dr Vernon Fernandes
wakwanza kuli kuhusiana na Chanall za Dijitall zinavyofanya kazi,baada
ya Rais kufungua Kituo Kikuu cha Kurushia matangazo ya Dijitall hapo
Rahaleo Mjini Zanzibar.wapili kulia ni Waziri wa Habari Utamaduni Utalii
na Michezo Said Ali Mbarouk.
Rais
wa Zanzibar Dk Ali Mohd Shein katikati akiwa katika picha ya pamoja na
Viongozi wa Wizara ya Habari Utamaduni Utalii na Michezo na Mainjinia wa
Ujenzi wa Kituo Kikuu cha Kurushia matangazo ya Dijitall hapo Rahaleo
Mjini Zanzibar.
…………………………………………………….
Na Khadija Khamis –Maelezo Zanzibar
SHIRIKA la Utangazaji Zanzibar
ZBC limetakiwa kuhakikisha kwamba linafanyakazi kwa ufanisi mkubwa
kulingana na mfumo uliopo hivi sasa.
Alisema kuwa wafanyakazi wa shirika hilo wameonakana wakifanya kazi kimazowea tu bila kufuata taratibu za kikazi.
Hayo yameelezwa leo na Rais wa
Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Ali Mohammed Shein
katika Uzinduzi wa Miundombinu ya Dijitali na Jengo la Studio ya Kisasa
Alisema kuwa kubadilika kwa watendaji kazi ni suala la lazima kutokana na mabadiliko makubwa yalioko duniani .
Dkt Shein alisema kuwa ZBC
wananchi wengi wanapiga kelele juu ya utendaji wa wafanyakazi wa ZBC
kutokana na vipindi vyao kutoridhisha na kukatika katika kwa matangazo
yao zaidi wakati wa taarifa ya habari.
Alisema kuwa Zanzibar inaheshima
yakekatika masuala ya Utangazaji kwani Redio nyingi za Nje
zinawatangazaji kutoka Zanzibar ambao ni mahiri katika masuala ya
Utangazaji.
Dkt Shein amesema kuwa hivi sasa
hatoweza kuvumilia tena kutokana na utendajihuo ambao hauridhishi hata
kidogo na hasa sasa tulivyoingia katika mfumo huu wa DIGITALI.
“Sitaki kuiona Serikali ambayo nnayoiongoza mie iwe ‘tiro’(mwisho) alisema Dkt Shein.
Alisema kuwa kuingia katika mfumo
mpya wa dijitali ni kazi kubwa lazima watendaji wafanyekazi kwa
mashirikiano na kuwe na uwiano baina yao ili kuweze kuwa na kiwango
ambacho kitaweza kuwajengea sifa wafanyakazi hao.
No comments:
Post a Comment