Shirikisho
la Ngumi la Kimataifa (IBF) katika bara la Afrika, Ghuba ya Uajemi na Mashariki
ya Kati linawaalika wafanyabishara wa kitanzania kuhudhuria mkutano wa mwaka wa
IBF/USBA utakaofanyika katika jiji la Berlin nchini Ujerumani kuanzia tarehe
Mei 21-25th, 2013.
Katika
mkutano huo wanachama zaidi ya 3000 wa IBF/USBA kutoka nchi zaidi ya 200
duniani watahudhuria.
Hii
ni fursa pekee kwa wafanyabishara wa Kitanzania kuweza kutumia mkutano huu
kutangaza biashara zao katika sekta mbalimbali hususan sekta ya Kitalii,
TEHAMA, usafirishaji wa bidhaa za kitanzania nje ya nchi pamoja na uwekezaji
katika sekta mbalimbali nchini.
Mkutano
wa mwaka wa IBF/USBA huwakutanisha wafanyabishara waliowekeza katika sekta
mbalimbaki za kiuchumi na hutoa fursa kubwa kwa wafanyabishara kujenga mitandao
mzuri wa biashara.
Rais
wa Rais wa IBF katika bara la Afrika, Ghuba ya Uajemi na Mashariki ya Kati
Mtanzania Onesmo Ngowi anawahimiza Watanzania kuchangamkia fursa hizi ili
waweze kufaidika kiuchumi,
Aidha,
Ngowi anawahamasisha wakuzaji wa mchezo wa ngumi pamoja na wale wanaofanya
shughuli za Branding (kukuza biashara) kuhudhuria mkutano huu na kujipatia
fursa mbalimbali za biashara.
Ngowi
ataongoza ujumbe nzito kutoka bara la Afrika, Ghuba ya Uajemi na Mashariki ya
Kati wakiwamo Mawaziri wa Michezo kadhaa kutoka nchi zilizo katika ukanda huu.
No comments:
Post a Comment