Na Gladness Mushi,Arusha.
Waziri
wa Wizara ya Viwanda na Biashara Dr.Abdallah Kagoda amesema kuwa
mipaka ya nchi imekuwa chanzo cha uingizwaji wa bidhaa ambazo ziko chini
ya viwango (feki) hali inayochangia kuleta athari kubwa kiuchumi na afya
za watu wanaotumia bidhaa hizo.
Aidha
waziri huyo ameeleza kuwa uingizaji wa bidhaa bandia nchini unatokana na
taasisi zinazoshughulikia masuala ya viwango vya ubora kutoimarika kiutendaji .
Akizungumza
katika ufunguzi wa Warsha iliyoandaliwa na shirika la dunia linalohusika na
mambo ya kuandaa viwango (ISO) wakishirikiana na shirika linaloshughulikia
viwango na ubora wa bidhaa nchini (TBS),warsha iliyokuwa ikijadili juu ya mfumo
wa uzalishaji kuanzia malighafi,bidhaaa,mtumiaji na taka inayotokana na bidhaa
hiyo ilivyo na athari katika mazingira yaani (Life Cycle).
“Mkutano
huu ni muhimu kwa nchi zinazoendelea kushiriki katika kuweka vigezo vya viwango
vya ubora na kujiaandaa kuvitimiza ili kuweza kuuza bidhaa katika soko la dunia
ili kuondokana na vikwazo katika uingizaji wa bidhaa zao kwenye soko hilo
kutokana na bidhaa kutokizi ubora wa kimataifa na teknolojia dhaifu
inayotumika kuanzia malighafi,bidhaa hadi usafirishaji” Waziri Kagoda
Kwa
upande wake Kaimu Mkurugenzi wa TBS Bwana Leandri Kinabo amesema kuwa mkutano
huo ni muhimu kwani unalenga kuweka mikakati ya viwango,na uzalishaji bora
unaozingatia ubora ili kushiriki kikamilifu katika soko la dunia (WTO)
ukizingatia kuwa Tanzania ni nchi mwanachama wa soko hilo .
Hivyo
amewataka wazalishaji kuzingatia utunzaji wa mazingira katika mfumo
mzima wa uzalishaji kuanzia malighafi,bidhaa,usafirishaji na utupaji wa taka
inayotokana na bidhaa hiyo (Disposal).
Baadhi
ya washiriki wa mkutano huo ni kutoka nchi za Afrika Mashariki,Ukanda wa Kusini
mwa Afrika (SADC) na pia unatarajia kuhudhuriwa na nchi za
Malaysia,India,China na Uingereza.
No comments:
Post a Comment