Miss Demokrasia Tanzania and Entertainment Co Ltd added 18 new photos.
HII NDIYO SHULE YETU YA WIKI HII TAREHE 20/7/2014.
kama unavyofahamu tena sisi wajibu wetu ni kujaribu kufuatilia kwa makini maendeleo ya wanafunzi, juu ya haki zao za msingi kisheria na Demokrasia ya Kweli. Shule hii ipo eneo la Vingunguti / Kipawa ni kwa mwendo kama wa dakika 10 kwa miguu toka barabara kubwa liendalo gongolamboto buguruni, ambapo jicho na darubini yetu ilipiga kambi kwa siri. Kati ya Mambo mazuri katika Shule hii ni pamoja na Wanafunzi Kupenda Utulivu wakati wote, wanafunzi hawa wanakuwa kila mmoja bize na masomo pamoja na kwamba wapo wengine ambao muda mwingine pia wanapata fulsa ya kupenya penya hapa na pale kwa kuchengana na walimu wao kwa tofauti ambazo ni za kimasomo.

Aidha Darubini yetu ilifanikiwa pia kufanya mazungumzo na baadhi ya
Wanafunzi na Walimu kuhusu Shule hiyo," Eh wewe kwani ni nani? Mpiga
Picha au? aliuliza mwanafunzi mmoja aliyekuwa ameketi kwenye kundi la
Wenziwe huku wakiendelea kupiga Stori, Wakati ilikuwa yapata majira ya
saa sita, wakati huo njaa pia zilikuwa zinaonekana kuwakwaza maana
vijembe navyo vilisikika vya uchokozi wao kwa wao, "wewe naye unataka
kuwa mwandishi wa habari, au unatafuta habari? njaa tu inakuwasha
tumboni muda huu, unamuuliza huyo mtu wa watu yeye nani kwani wewe
unataka awe nani? je kama ni mwandishi wa habari anatafuta habari,
unataka kumpa hizo habari? yaani watoto wale kiboko, mie " mi nataka
nimpe habari akauze vizuri kama kweli yeye anatafuta habari, wewe mkaka
uje unipige picha, kwani ni bure au na hela? na hela nikamjibu ili
nisije nikaharibu kabisa dili lenyewe, " je ni shilingi ngapi? " ni mia
tano ila nikikuletea utanipa sawa," oh kumbe Simple tu, aisee niphotoe
haraka kabla Walimu hawajaleta zao, maana kuna mmoja huyo mnokon kweli
utadhani nini, hataki hata sisi Wanafunzi tupige picha za kumbukumbu
tunapokuwa kwenye pozi zetu, sijui yeye alipokuwa anasoma wakati wake
hapakuwa na kamera? eti wewe mpiga picha ni Sahihi kupiga picha sisi
tukitaka za kumbukumbu au ni makosa?
Swali lake ilikuwa mtego sana kwangu, lakini baada ya kutafakari nikampa " kwani Shule ni ya Nani? Shule ipo kwa ajili ya Walimu au Shule kwa ajili ya Wanafunzi? nikampa na hiyo" Lakini wakati zoezi linaendelea mara yule asiyependa wanafunzi wapige picha akatokea wakaanza kutoka mbio, nikajaribu kuwasihii wamsikilize mwalimu wao maana alikuwa sasa anawaita kwa asira, kama unavyofahamu tabia za wanafunzi, wakimuona mwalimu wanageuza mgongo ili wasionekane sura, kwa hiyo mimi nikawambia hapa msikimbie nyie msikilizeni tu na mimi hapa nitajaribu kuwatetea maana sidhani kama kuna kosa kwenu kupiga picha za ukumbusho baina yenu, isipokuwa kosa ni kujaribu/kupiga picha chafu.
basi baada ya kuitikia wito wa mwalimu wao, msamaha wa mwalimu huyo kwanza kabisa ilikuwa ni wote kupiga magoti kwenye eneo la jua kali,(Wakati wanapigishwa magoti tayari ailitwa asikari kuja kutazama kama wanatimiza adhabu, baada ya hapo huyo mwalimu akaniita na mimi na kutoa oda picha zote zilizoko ndani ya kamera zifutwe, " Askari ulikuwa wapi wakati hawa Vitoto wanapiga piga picha, ili lingine litazame hata akili hamnazo kabisa lakini kwa Picha, Hakikisha Picha zote zilizomo kwenye hiyo kamera zimefutwa. Inaendelea katika ukurasa wetu wa mtandao wa Blogs: www.missdemokrasia.blogspot.com/ www.baloziwademokrasiatanzania.blogspot.com

No comments:
Post a Comment