TAN
Bayport
Kikoa
Myway entertainment
FORE PLAN CLINIC
MPINGA CUP 2016
Mashujaa Fm 89.3, Lindi
Wednesday, March 30, 2016
Profesa Muhongo: Kamilisheni miradi ya umeme vijijini kwa wakati
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo akizungumza na watendaji wa wizara pamoja na kampuni ya CCC International Nigeria, (hawapo pichani) lengo likiwa ni kupokea taarifa ya utekelezaji wa miradi ya umeme vijijini ya kampuni hiyo katika mkoa wa Manyara.
Meneja mradi wa Kampuni ya CCC International Engineering Nigeria, Zhang Jiangaang (Mwenye shati jeupe) akiwasilisha ripoti ya maendeleo ya usambazaji wa umeme vijijini inayosimamiwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) awamu ya pili.
Na Latifah Boma Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo amewataka wakandarasi wanaotekeleza miradi ya umeme vijijini kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) awamu ya pili kufanya kazi kwa kasi zaidi ili umeme uweze kuwafikia walengwa kabla ya mwezi Juni mwaka huu.Akizungumza na watendaji kutoka kampuni ya CCC International Nigeria Limited, inayosambaza umeme katika mkoa wa Manyara, Profesa Muhongo alisema kuwa hajaridhishwa na kasi ya kampuni hiyo katika utekelezaji wa miradi ya umeme katika wilaya ya Simanjiro ambapo hakuna wateja waliounganishiwa umeme. Pia, Profesa Muhongo amelitaka Shirika la Umeme Nchini (TANESCO) kufanya kazi kwa karibu na wakandarasi hao katika kutatua changamoto zinazowakabili ili waweze kukamilisha miradi hiyo kwa wakati. Aliwataka mameneja wa TANESCO kuongeza juhudi katika kazi zao ikiwa ni pamoja na makusanyo, utatuaji wa changamoto na uunganishaji wa umeme kwa wateja, na kusisitiza kuwa meneja atakayeshindwa kutekeleza majukumu yake ataondolewa katika nafasi yake. Awali, akielezea changamoto katika utekelezaji wa miradi ya umeme meneja mradi kutoka CCC International Nigeria Limited.Zhang Jiangaang, alieleza kuwa wamekuwa wakiibiwa vifaa vyao vya kazi kutokana na kuwepo kwa usalama mdogo hivyo kupelekea kutokamilisha mradi kwa wakati kutokana na hasara wanayoipata.
No comments:
Post a Comment
Newer Post
Older Post
Home
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment