TAN
Bayport
Kikoa
Myway entertainment
FORE PLAN CLINIC
MPINGA CUP 2016
Mashujaa Fm 89.3, Lindi
Wednesday, March 30, 2016
China yaonesha nia ya kuwekeza kwenye sekta ya nishati
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia nishati Dk. Mhandisi Juliana Pallangyo (kulia) akisalimiana na mmoja wa wajumbe kutoka kampuni uzalishaji wa makaa ya mawe ya Shenhua Ningxia Group Co. Limited kutoka China. (kushoto). Katikati ni Mwakilishi kutoka Umoja wa Wafanyabiashara katika Jamhuri ya Watu wa China nchini Tanzania, Lin Zhiyong.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia nishati, Dk. Mhandisi Juliana Pallangyo (kulia) akielezea fursa za uwekezaji katika sekta ya nishati nchini. Kushoto ni Mwakilishi kutoka Umoja wa Wafanyabiashara katika Jamhuri ya Watu wa China nchini Tanzania Lin Zhiyong.
Mwakilishi kutoka Umoja wa Wafanyabiashara katika Jamhuri ya Watu wa China nchini Tanzania, Lin Zhiyong (pichani) akisisitiza jambo katika kikao hicho.
Sehemu ya ujumbe kutoka nchini China ukifuatilia majadiliano mbalimbali yaliyokuwa yanaendelea katika kikao hicho.
Mchimbaji wa Makaa ya Mawe kutoka Nchini Tanzania, Sara Masasi akielezea uzoefu wa kampuni yake katika uzalishaji wa makaa ya mawe.
Na Greyson Mwase, Dar es Salaam
Wawekezaji kutoka katika makampuni yanayojihusisha na uzalishaji wa nishati ya umeme kutoka nchini China, wameeleza nia ya kuwekeza kwenye sekta ya nishati nchini ili iweze kuwa na mchango mkubwa katika ukuaji wa uchumi.
Waliyasema hayo katika kikao na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia masuala ya nishati Dk. Mhandisi Juliana Pallangyo pamoja na wataalam kutoka Wizara ya Nishati na Madini pamoja na taasisi mbalimbali ikiwa ni pamoja na Shirika la Umeme Nchini (TANESCO), Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC) na Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA)
Akizungumza katika kikao hicho Mwakilishi kutoka Umoja wa Wafanyabiashara katika Jamhuri ya Watu wa China nchini Tanzania Lin Zhiyong, alisema kuwa nia ya makampuni yanayojishughulisha na uzalishaji wa nishati ya umeme ni kubaini fursa zilizopo katika sekta ya nishati nchini kabla ya kuja kuwekeza rasmi
Aliongeza kuwa ujumbe maalum wa wawekezaji kutoka nchini China unatarajiwa kuwasili nchini mapema wiki ijayo kwa ajili ya kupata taarifa mbalimbali zenye kubainisha fursa za uwekezaji nchini ikiwa ni pamoja na mpango kabambe (master plan), sera, na mpango mkakati katika sekta ya nishati, kabla ya kusaini makubaliano ya awali kwa ajili ya uzalishaji wa nishati ya umeme.
Zhiyong alisisitiza kuwa wawekezaji kutoka China wako tayari kushirikiana na wawekezaji wa ndani ya nchi kwenye uzalishaji wa nishati ya umeme ili taifa liweze kupata nishati ya uhakika kwa ukuaji wa uchumi wa nchi.
Wakati huo huo, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia nishati Dk. Mhandisi Juliana Pallangyo alishukuru ujumbe huo na kueleza kuwa fursa za uwekezaji kwenye sekta ya nishati ni nyingi na kuwataka kuchangamkia fursa hizo.
“Wananchiwanahitaji nishati ya uhakika ambayo nikichocheo cha ukuaji wa uchumi wa nchi,hivyo tunawakaribisha kuwekeza katika uzalishaji wa nishati ya umeme kwakuwa tuna vyanzo vingi kama vile gesi, jotoardhi, makaa yamawe, jua, upepo n.k,” alisisitiza Dk. Palangyo.
No comments:
Post a Comment
Newer Post
Older Post
Home
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment