TIMU
ya Afya Sports Bara na Afya Sports Zanzibar zimetoka sare bao moja kwa
moja katika mchezo uliofanyika jana katika Uwanja wa Hospitali ya Taifa
ya Muhimbili (MNH) jijini Dar es salaam.
Timu
ya Afya Sports Zanzibar ilikuwa ya kwanza kutikisa nyavu na bao la
kwanza lilifungwa na Haji Abdalah kwenye dakika ya 22 kipindi cha
kwanza.
Katika
kipindi cha pili timu ya Afya Bara ilifurukuta na kurejesha bao
lililofungwa na Mesa, hatua iliyopelekea timu hizo kutoka sare ya bao
moja kwa moja.
Katika
hatua nyingine, timu ya Netibili ya Afya Bara imeifunga mabao 30 -29
timu ya Netiboli ya Afya Zanzibar kwenye mchezo uliofanyia kwenye Uwanja
wa Netiboli iliyopo ndani ya Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH).
Mchezo
huo ni Tamasha la Pasaka ambalo hufanyika kila mwaka kati ya Watumishi
wa Sekta ya Afya Zanzibar na Watumishi wa Sekta ya Afya Bara kwa lengo
la kuendeleza undugu na ushirikiano.
Mchezaji
wa timu ya Afya Bara, Drisa akimtoka mchezaji wa Afya Zanzibar, Hassan
Abdallah “Kimti” katika mchezo wa tamasha la Sikukuu ya Pasaka. Katika
mechi hiyo timu hizo zilitoshana nguvu sawa. Afya Zanzibar 1-1 Afya
Bara. Mchezo huo ulifanyika jana kwenye viwanja vya Hospitali ya Taifa
ya Muhimbili (MNH).
Wachezaji wa timu ya soka Afya Bara na Zanzibar wakiwa katika picha ya pamoja baada ya mchezo.
Wachezaji
wa Netiboli ya Afya Zanzibar wakiwa katika picha ya pamoja baada ya
kumalizika kwa mchezo. Afya Bara imeifunga Afya Zanzibar mabao 30-29.
Mchezo huo umefanyika jana kwenye viwanja vya Hospitali ya Taifa ya
Muhimbili (MNH).
No comments:
Post a Comment