Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee,
Dk. Hamis Kigwangalla akizungumza na wanafunzi wa sekondari (hawapo
pichani) juu ya ugonjwa wa Endometrosis katika semina hiyo kutoa elimu
ya ugonjwa iliyoratibiwa na Miss Tanzania 2001, Millen Magese ambaye ni
Mhanga wa Ugonjwa huo leo jijini Dar es Salaam.
Mkuruenzi Millen Magese Foundation na Miss Tanzania 2001, Millen
Magese akizungumza wakati wa semina ya wanafunzi wa sekondari juu ya
ugonjwa wa Endometrosis ambapo yeye ni mhanga wa ugonjwa huo
iliyofanyika leo katika shule sekondari Tulian Jijini Dar es Salaam.
Naibu
Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, watoto na Wazee,
Dk. Hamis Kigwangalla akiwa katika picha ya pamoja na Miss Tanzania
2001, Millen Magese na wageni walikwa katika semina ya utoaji wa elimu
ya ugonjwa wa endometrosis leo jijini Dar es Salaam.
Na:Mwandishi Wetu,
IMEELEZWA kuwa kutibu ugonjwa wa Endometrosis ni gharama kubwa na serikali pekee yake haiwezi kushughulikia tatizo hilo.
Ugonjwa huo huwapata wanawake wakati wa hedhi na kufanya mwanake kukosa furaha na kutibu kwake ni gharama kubwa.
Akizungumza
na leo katika semina kutoa uelewa kwa wasichana 400 iliyoandaliwa na
Taasisi ya Miss Tanzania 2001 Millen Magese, Naibu Waziri wa Wizara ya
Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamis Kigwangalla
amesema kuwa ugonjwa wa Endometrosis unasababisha ugumba kwa wanawake.
Amesema
kugundua ugonjwa huo unachukua kati ya miaka sita hadi 10 na kati ya
wanawake 100 wenye ugonjwa huo nusu hawawezi kupata watoto.
Dk.Kigwangalla
amesema kutambua ugonjwa huo kwa wataalam inachukua miaka saba hadi 10
hivyo kunahitajika elimu hata maeneo vijijini wanawake wanaweza wanaugua
lakini hawajui.
“Wahenga
wanasema raha ya mwanamke na kuzaa mtoto wake mwenye hivyo kuwa na
ugonjwa unafanya mwanamke akose furaha katika maisha yake”amesema
Kigwangalla.
Mkurugenzi
wa Millen Magese Foundation,Miss Tanzania 20O1, Millen Magese amesema
kuwa amefanyiwa operesheni mara 13 na kuamua kutoa elimu juu ya ugonjwa
huo.
Amesema kuwa wanawake wengi wanasumbuliwa na ugonjwa huo lakini wanasema ni siri wakati ni ugonjwa wenye maumivu makali..
No comments:
Post a Comment