TAN
Bayport
Kikoa
Myway entertainment
FORE PLAN CLINIC
MPINGA CUP 2016
Mashujaa Fm 89.3, Lindi
Tuesday, March 29, 2016
COSATO CHUMI APONGEZWA NA WANANCHI WA JIMBO LA MAFINGA MJINI
Na Fredy Mgunda,Iringa
Wananachi wa maeneo mbalimbali ya jimbo la mafinga mjini wamesema utaratibu wa mbunge wao Cosato Chumi kwa kwenda kutembelea maeneo yenye kero ni dalili njema zinazoonyesha kuwa hawakufanya makosa kumchagua kuwa mbunge wao na kuongeza hatadanganywa na watendaji walioko chini yake tatizo linalosababisha viongozi wengi kutoa maamuzi yasiyo sahihi na yanayoendelea kuiathiri jamii.
Mbunge wa jimbo la Mafinga mjini mkoani Iringa Cosato Chumi akiwa na
balozi wa korea mh Geum-young song wakipata picha ya pamoja baada ya maongezi ya muda mrefu.
Aidha wananchi hao wamempongeza mbunge wao kwa juhudi anazo zifanya za kukutana na watadau mbalimbali kwa ajili ya kuwaletea maendeleo wananchi wa jimbo lake.
“Tumeona mbunge wetu akikutana na mabalozi wa nchi tofauti tofauti na wanazungumzia maendeleo ya jimbo la mafinga mjini mfano hivi karibuni mbunge wetu alikuwa na balozi wa korea mh Geum-young song tunajua kunakitu tutapata kutoka kwa balozi huyo”. Walisema wananchi
Kwa upande wake mbunge wa jimbo la Mafinga mjini mkoani Iringa Cosato Chumi ameanza kutimiza ahadi zake kwa wananchi wa jimbo la Mafinga mjini kwa kufanya ziara ya kutambua matatizo ya wananchi wake na kutambua nini vipaumbele vyao.
Chumi alisema kuwa lengo la kutimiza ahadi yake hiyo ni kama njia ya kuwashukuru wana Mafinga mjini kwa kumchagua katika uchaguzi uliofanyika hivi karibuni pia kutimiza ahadi mbali mbali binafsi ambazo alizitoa wakati akiomba kura kwa wananchi.
Alisema ataendelea kutimiza ahadi binafsi zilizotolewa wakati kampeni kulingana na uwezo wake na zile za kitaifa ambazo zipo katika Ilani ya CCM atahakikisha anaikumbusha serikali ya CCM ili kutimiza ahadi hizo kwa wakati.
“Ndugu zangu wananchi mbali ya kuwa ubunge wangu ni wa mwaka mmoja ila tayari mimeanza kutimiza ahadi bila ya kuchelewa na ninawahakikishieni sita waangusha nitaendelea kufanya hivyo zaidi mniombee uzima”.alisema Chumi
Mbunge huyo ameongeza kuwa hivi karibuni anatarajia kupokea msaada wa kuchimbiwa visima vitano kwenye shule za sekondari na msingi za jimbo hilo ambapo visima viwili kwa sekondari na vitatu vya shule ya msingi,msaada huo umetoka kwa ubalozi wa korea mh:Geum-young song.
“Leo nilialikwa lunch na balozi wakorea mh:Geum-young song na tumeongea mambo mengi lakini kubwa nimeahidiwakuchimbiwa visima vitano kwenye shule za msingi na sekondari zilizopo kwenyejimbo la mafinga mjini mungu ni mwema jambo hili likifanikiwa litatusaidia kuwapunguziaadha wanafunzi wetu”.alisema Chumi.
No comments:
Post a Comment
Newer Post
Older Post
Home
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment