Mwanasaikolojia
Anti Sadaka akitoa Mada kwenye Mafunzo ya ujasiriamali kwa wanawake wa
Mkoa wa Dodoma yanayoendeshwa na Taasisi ya Manjano Foundation
yanaoendelea kwenye ukumbi wa LAPF House.
Mwanasaikolojia
Anti Sadaka amewafunda wanawake wa Dodoma wanaoshiriki mafunzo ya
ujasiriamali ya kujikita katika biashara ya Vipodozi vya LuvTouch
Manjano. Mafunzo hayo yanaendeshwa na wataalamu kutoka taasisi ya
Manjano Foundation na mkufunzi wa maswala ya Biashara mjini Dodoma
yanayoendelea kwa wiki nzima.
Anti
Sadaka amewataka wanawake hao kujitambua kwa lengo la kufikia malengo
yao waliojiwekea. Akieleza zaidi katika semina hiyo amewataka wanawake
hao kujitambua wao ni nani, wajiamini, watambue vyeo vyao katika
familia, wana nafasi gani kwenye jamii inayowazunguka, kufanya kazi kwa
bidii na kudumisha nidhamu yao kwa kila wakifanyacho kwa lengo la
kufikia malengo yao.
Pia amewaasa wanawake walioshiriki mafunzo hayo mjini Dodoma kuchangamkia FURSA zinazowazunguka. Semina
hiyo inawanufaisha wanawake wa Dodoma kwa lengo la kuwaongezea kipato
na pia kuweza kujiajiri ili kujikwamua na tatizo la ukosefu wa ajira.
No comments:
Post a Comment