Mbunge
wa jimbo la Kinondoni Maulid Mtulia akizungumza na wandishi wa habari
juu ya kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi ya mbunge wa jimbo la
kinondoni haina madai ya msingi na hivyo mahakama ilistahili
kuitupilia mbali badala ya kuendelea kuipiga kalenda leo jijini Dar es
Salaam.
Wakili
mshitakiwa Juma Nassoro akizungumza na waandishi wa habari leo jijini
Dar es Salaam. juu ya kesi hiyo kusikilizwa na Jaji Lugano Mwandambo kwa
njia ya maandishi ilipangwa kutolewa maamuzi leo, ila kwa bahati mbaya
jaji huyo hakuweza kufika mahakamani kulingana na kupangiwa
kushughulikia kesi zingine za uchaguzi mkoani Kilimanjaro. Kulia ni
.Mbunge wa jimbo la Kinondoni Maulid Mtulia.
Mbunge wa jimbo la Kinondoni Maulid Mtulia akitoka Mahakani hapo mara baada ya kesi hiyo kuahilishwa.
(Picha na Emmanuel Massaka wa Globu ya Jamii)
KESI
ya kupinga matokeo ya uchaguzi ya Mbunge wa jimbo la Kinondoni Maulid
Mtulia(CHADEMA) iliyofunguliwa na aliyekuwa Mbunge wa jimbo hilo, Idd
Azzan imeshindwa kutolewa maamuzi hii leo kama ilivyokuwa imepangwa na
mahakama kuu ya Tanzania.
Juma
Nassoro ambaye ni wakili wa mshitakiwa Maulid Mtulia ambaye ni Mbunge wa
Kinondoni amesema kuwa baada ya kesi hiyo kusikilizwa na Jaji Lugano
Mwandambo kwa njia ya maandishi ilipangwa kutolewa maamuzi leo, ila kwa
bahati mbaya jaji huyo hakuweza kufika mahakamani kulingana na kupangiwa
kushughulikia kesi zingine za uchaguzi mkoani Kilimanjaro, ambapo
amemuaomba msajili kumpanga jaji mwingine atakaye andika hukumu ya kesi
hiyo, na hivyo wameambiwa kurudi tena kesho mahakamani kwa ajili ya
kupangiwa tarehe nyingine.
Kwa
upande wa Mbunge Mtulia anayekabiliwa na kesi hiyo ameeleza
kusikitishwa na kilichotokea kwa kile alicho dai kuwa kesi hiyo haina
madai ya msingi na hivyo mahakama ilistahili kuitupilia mbali badala ya
kuendelea kuipiga kalenda.
No comments:
Post a Comment