TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Tuesday, September 17, 2013

TANZANIA YACHAFULIWA MALAWI

Posted: 16 Sep 2013 04:58 AM PDT


Na Rachel Balama
TANZANIA imekanusha habari zilizoandikwa na gazeti moja nchini Malawi "Malawi News" na kudai raia wa Malawi waishio nchini Tanzania, wanaishi kwa wasiwasi mkubwa wakihofia hali ya hatari kutokana na ubaguzi unaofanywa na Watanzania,  Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Msemaji wa Serikali na Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo, Bw. Assah Mwambene, alisema habari hiyo haina ukweli wowote kwani hakuna raia wa Malawi aliyedhalilishwa,  kubakwa wala kufanyiwa vitendo vyovyote vya ukatili.

Alisema habari hiyo imelenga kuidhalilishaTanzania ambapo Septemba1 4, mwaka huu, walik amatwa wahamiaji haramu 1,030 toka nchini Malawi ambao hawakuwekwa ndani badala yake walihojiwa, kupewa fomu ili kuhalalisha ukaazi wao. "Habari iliyoandikwa na gazeti hili haiwezi ku vumilika hata kidogo, Serikali yaTanzani ahaiwezi kufananishwa na vitendo vya ubaguzi vilivyo kuwa vikifanywa nchini Afrika Kusini. "Tayari wahamiaji 25,000 kutoka nchi za Burund i, Rwanda, Uganda, Zimbabwe na Congo DRC, walikamatwa katika Mikoa ya Kigoma, Mbeya, Rukwa ,Geita na kwingineko ambapo wote wa lirudishwa makwao,"al isema Bw, Mwambene.

Aliongezakuwa, operesheni ya kuwakamata na kuwarudisha ma kwao wahamiaji wanaoishi nchini bila vibali siku toka Malawi pekee, ina tekelezwa kutokana na agizo alilotoa Rais Jakaya Kikwete baada ya kutoa wiki mbili za kuwataka waond oke kwa hiari yao. Septemba14,mwa ka huu, gazeti hilo liliandika habari inayosema"Wa malawi nchini Tanzania wanaishi kwa kujificha kutokananahali yahatari nahadis asa, mmoja wao amebakwa wakilinganisha matukio hayo na ubaguzi uliokuwa ukifanyika AfrikaKusini".
Bw. Mwa mbene amelitaka gazeti hilo kusahihisha taarifa yake na kuomba radhi kwa upotoshaji huo kwani habari hiyo ni sawa na matusi kwaTanzani.

No comments:

Post a Comment