Wafugaji wa kijiji cha Mvomero-Morogoro wamewavamia wenzao Wakulima na kuwapiga, na kisha kusababisha Mejeruhi ya watu wanne(4) kutokana na mzozo unaoendelea kati ya wafugaji(wamaasai) na wakulima kutika kijiji hicho cha Kambala Mvomero, Pia wananchi wa kijiji hicho wameilaumu serikali kwa kushindwa kutoa suluhisho la mzozo huo baina ya Wafugaji na Wakulima ambalo kwa sasa linazidi kukua na limekua swala la mda mrefu sasa. Taarifa zinasema kuwa Wafugaji hao waliamua tu kuvamia wenzao wakulima na kuwapiga pasipo sababu ya msingi na huku Polisi wa eneo hilo kushindwa kuchukua hatua inayotakiwa mapema. Mkuu wa wilayani hapo (Mvomero) Anthony Mtata amewaomba wananchi hao waathirika wa tukio hilo kutojichukulia hatua mkononi na kuwahakikishia wakulima hao kwamba, waliohusika na tukio hilo lazima watiwe nguvuni.
Utangulizi | ||||||||||||||||||||||
Wilaya ya Mvomero ni moja kati ya Wilaya 5 (tano) za Mkoa wa Morogoro. Wilaya hii imeanzishwa mwaka 2002 na ina jumla ya kilomita za mraba 7,325 sawa na 9.98% ya eneo la Mkoa. Wilaya ina jimbo moja la Uchaguzi wa Ubunge la Mvomero linaloanzia Mgeta kwenye Milima ya Uluguru hadi Turiani kwenye Milima ya Nguu. Wilaya inapakana na Wilaya ya Kilindi mkoani Tanga kwa upande wa Kaskazini na Wilaya ya Kilosa kwa upande wa Magharibi. Kwa upande wa Kusini inapakana na wilaya Morogoro na kwa upande wa Kaskazini Mashariki inapakana na wilaya za Bagamoyo na Handeni.
| ||||||||||||||||||||||
UMBILE LA ARDHI | ||||||||||||||||||||||
Umbile la Wilaya ni kama mwezi mchanga unaoambaa ambaa Manispaa ya Morogoro kuelekea Kaskazini. Kijiografia Wilaya imegawanyika katika nyanda tatu kama ifuatavyo:-
• Nyanda za juu ( Highland and Mountainous Zone):
Nyanda hizi hasa ni zile za milima ya Uluguru na Ungulu. Eneo hili limechukua 25% ya eneo la Wilaya. Nyanda hizi zipo kwenye mwinuko wa mita 1200 – 2000 kutoka usawa wa bahari. Nyanda hizi zinafaa kwa mazao ya biashara kama vile; kahawa, Hiliki na mazao ya chakula kama mahindi, maharage, mboga, ndizi, viungo na matunda.
• Nyanda za chini (Low and Semi Mountainous Zone):
Nyanda hizi zipio kwenye mwinuko wa mita 800 hadi 1200 kutoka usawa wa bahari. Nyanda hizi hustawisha mazao kama mahindi, mihogo, mtama kwa chakula na mazao ya biashara ni Miwa na Alizeti.
• Nyanda za Tambarare (Savannah Zone):
Nyanda hizi zipo kwenye mwinuko (altitude) wa mita 600 – 800 kutoka usawa wa bahari. Mazao yanayostawi kwenye nyanda hizi ni mpunga, Mahindi, na Mihogo kama mazao ya chakula, na mazao ya biashara ni Miwa, Pamba na Katani.
| ||||||||||||||||||||||
IDADI YA WATU | ||||||||||||||||||||||
Kutokana na sensa ya mwaka 2002, Wilaya ina wakazi wapatao 260,525 kati yao wanaume ni 131,256 na wanawake 129,269. Jumla ya Kaya katika Wilaya ni 58,314 zenye wastani wa watu 4.5 kwa kila Kaya. Ongezeko la watu kwa mwaka ni 2.6%.Wilaya inaonyesha kuwa na nguvu kazi ya watu 142,755 sawa na 54.8% ya wakazi wote 260,525.
| ||||||||||||||||||||||
Hali ya Hewa | ||||||||||||||||||||||
Kwa kawaida Wilaya inapata mvua mara mbili kwa mwaka. Mvua za vuli, ambazo huanza mwezi Oktoba hadi Januari. Mvua za masika, ambazo huanza mwezi Februari hadi Mei/Juni. Wilaya hupata wastani wa 1900mm za mvua kwa mwaka. Hali ya joto ni nyuzi 29 0 C
| ||||||||||||||||||||||
Utawala | ||||||||||||||||||||||
Halmashauri ina jimbo moja la uchaguzi ambalo ni Mvomero na Bw Paul C. Kiyumbi ndiye Mwenyekiti wa Halmashauri na Bibi S. Linuma ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri.
| ||||||||||||||||||||||
Sekta ya Kilimo | ||||||||||||||||||||||
Hali ya Kilimo
Kilimo ni uti wa mgongo wa uchumi wa Wilaya ya Mvomero. Asilimia 84.1% ya wakazi wa Wilaya wanajishughulisha na Kilimo na ufugaji. Eneo linalofaa kwa kilimo ni Hekta 549,375 na eneo linalolimwa ni Hekta 247,219 sawa na 45% ya eneo lote linalofaa kwa kilimo. Eneo linalofaa kwa kilimo cha umwagiliaji ni Hekta 20,579 lakini eneo linalomwagiliwa ni Hekta 5,281 . Idadi ya wakulima ni 142,755 ambao kati yao wanaume ni 71,922 na wanawake ni 70,833. | ||||||||||||||||||||||
Maeneo ya uzalishaji | ||||||||||||||||||||||
Katika kutekeleza mpango huu, Halmashauri iLiainisha maeneo maalumu ya kuanzia katika mpango huu kwa mwaka 2007/2008.
Maeneo yamegawanywa katika Kanda tano, zenye Kata kumi na moja (11) na vijiji 44 kati ya vijiji 132 vya Wilaya ya Morogoro, Mazao yaliyohusishwa ni Mpunga, Mahindi na jamii ya mikunde. | ||||||||||||||||||||||
Upatikanaji wa pembejeo.
| ||||||||||||||||||||||
Pembejeo zilipatikana vizuri katika maduka ya mawakala wa pembejeo walioko mjini. Pembejeo zenye ruzuku pia upatikanaji wake ulikuwa mzuri, wakulima walipata mahitaji yao kupitia mawakala.
Pembejeo za ruzuku zilizopatikana ni mbolea aina ya urea tani 76, DAP tani 20 na mbegu za mahindi 2.2. Ambazo zilinunuliwa na mawakala na kuuzwa kwa wakulima. Wakulima walipata pembejeo kupitia mawakala waliopo vijijini na mjini.Vile vile wakulima katika vijiji 15 vya wilaya waliweza kuzalisha mbegu bora za mahindi tani 10 na kuwauzia wakulima wenzao kwa bei nafuu .Hii iliwezekana baada kupata mafunzo ya kuzalisha mbegu bora chini ya mradi wa ASDP.
| ||||||||||||||||||||||
Ushirika na Masoko | ||||||||||||||||||||||
Hali ya Ushirika:
Shughuli za Ushirika katika Wilaya ni za muhimu kwa kuzingatia kuwa idadi kubwa ya wakazi wa Wilaya ya Mvomero ni Wakulima wanaotegemea Kilimo na shughuli za biashara ndogondogo. Hata hivyo, ustawi wa vyama vya kilimo/Mazao bado sio wa kuridhisha japokuwa uanzishaji wa vikundi vya uzalishaji umekuwa ukijitokeza katika baadhi ya maeneo.
Pamoja na mikakati ya kuhakikisha Ushirika unawanufaisha Wananchi, huduma hii kwa sasa inatolewa na vyama 22. Vyama 17 vikiwa ni vya Ushirika wa Akiba na Mikopo, chama kimoja (1) kikiwa kinajishughulisha na Kilimo cha Mbogamboga na kuuza Pembejeo Mgeta. Chama kimoja (1) kinajishughulisha na Kilimo cha umwagiliaji Dakawa. Vyama viwili ambavyo ni Laramatak cha Kambala ni chama cha Ushirika wa wafugaji na Turiani AMCOS ambacho ni chama Ushirika cha Kilimo. Hivi ni vyama ambavyo tayari vimesajiliwa.
Vilevile kuna vyama 2 vya Ushirika wa Akiba na Mikopo kutoka Maskati na Melela viko kwenye mchakato wa kusajiliwa na kimoja cha ufugaji wa Mbuzi wa Maziwa kutoka Mgeta nacho kiko katika mchakato wa kusajiliwa.
Vyama vya Ushirika vya Akiba na Mikopo
Wilaya ina jumla ya vyama vya Akiba na Mikopo 17 ambavyo vina jumla ya wanachama 6726, Me 4597, Ke 2129 vikiwa na Hisa 435,091,000/=, Akiba 473,790,000/= na Amana 411,622,000/=. Pia vimeweza kutoa Mikopo yenye thamani ya Tshs. 5,177,457,000/= ."Hali Halisi angalia Jedwali A"
Mbali na kuwa na SACCOS 17, Wilaya ina Vyama 5 (vitano) vya Ushirika ambavyo vinajishughulisha na kilimo cha mbogamboga, maduka, umwagiliaji, kilimo cha nafaka na ufugaji. Vyama hivi vina jumla ya wanachama 961, Me 760 na Ke 201. Pia vina Hisa zenye thamani ya Tshs. 9,542,000/=
|
No comments:
Post a Comment