Na Eliasa Ally, Iringa
SIKU chache baada ya kuandika habari ya ukatili wa kutisha dhidi ya mwalimu anayedaiwa kuwalawiti wanafunzi wanne mkoani Iringa, mtuhumiwa huyo amekamatwa na yupo katika mikono ya polisi. Mwalimu huyo anafundisha katika Shule ya Sekondari Wanging'ombe, iliyopo Wilaya Mpya ya Wanging'ombe, mkoani Njombe, Bw. Mwasile Cletus (31).Miongoni mwa wanafunzi waliofanyiwa kitendo hicho mmoja ana miaka10(jina linahifadhiwa),ambaye anasoma darasa la nne katika Shule ya Msingi Chemchem, mjini humo.
Akizungumza, Kamanda wa Polisi mkoani Iringa,Ramadhan Mungi ,alisema mtuhumiwa huyo alikamatwa Septemba 13 mwaka huu, saa 10 jioni, akiwa kwenye nyumba aliyokuwa akiishi eneo la Don Bosco, mjini humo jirani na Chuo cha Mkwawa ambako anasoma.
"Mtuhumiwa ni mwanafunzi wa Mwaka wa Kwanza katika Chuo cha Mkwawa, anatuhumiwa kuwalawiti wanafunzi wanne baada ya kuwadanganya kuwa atawapa sh. 200 kila mmoja ili wasitoe siri hiyo kwa wazazi wao," alisema. Alisema mwanafunzi mmoja wapo kati ya waliolawitiwa, ndiye aliyewaongoza polisi hadi nyumbani kwa mshtakiwa na kuwaonesha chumba walichofanyiwa kitendo hicho .
Aliongeza kuwa,upelelezi wa kesi hiyo umekamilika na jalada lake limetumwa kwa Mwanasheria Mkuu w a Serikali ili kutoa uamuzi kama mtuhumiwa huyo afikishwe mahakamani kujibu tuhuma zinazomkabili za kuwalawiti wanafunzi. Wakizungumza kwa nyakati tofauti,baadhi ya wakazi wa eneo la DonBosco, Kata ya Mkwawa, walisema kama itabainika mtuhumiwa alifanya vitendo hivyo ,atakuwa ameidhalilisha taaluma y a ualimu ambayo inaheshimika duniani kote.
Baadhi ya Wahadhiri wa chuo hicho ambapo hawakutaka majina yao yaandikwe gazetini, walisema kuwa mwanafunzi wao atashindwa kuendelea na masomo chuoni hapo.
No comments:
Post a Comment