TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Tuesday, September 17, 2013

SIMBA, MTIBWA ZAINGIZA MIL. 95/-



MECHI ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kati ya Simba na Mtibwa Sugar iliyochezwa katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam imeingiza sh. 95,080,000.Katika mechi hiyo, Simba ilitoka kifua mbele baada ya kuifunga Mtibwa mabao 2-0

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na Ofisa Habari wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Boniface Wambura, watazamaji 16,507 walikata tiketi kushuhudia mechi hiyo.  Alisema viingilio katika mechi hiyo vilikuwa sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000 huku kila klabu ikipata mgawo wa sh. 23,018,077.45 wakati Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa ni sh. 14,503,728.81.

Wambura alisema mgawo mwingine wa mapato hayo ni asilimia 15 ya uwanja sh. 11,704,107.18, tiketi sh. 2,548,890."Gharama za mechi sh. 7,022,464.31, Kamati ya Ligi sh. 7,022,464.31, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 3,511,232.15 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 2,730,958.34," alisema.
Posted: 16 Sep 2013 05:25 AM PDT

Na Mwandishi Wetu
WAKATI homa ya shindano la Redd's Miss Tanzania ikiwa inapanda kwa washiriki wote, mrembo Prisca Clement juzi usiku amefanikiwa kutwaa taji la Redd's Miss Tanzania Talent lililofanyika katika hoteli ya Giraffe iliyopo Kunduchi, Dar es Salaam.

Kutokana na ushindi huo, Prisca ambaye anatokea Sinza akiwakilisha Kanda ya Kinondoni, amefanikiwa kuingia katika hatua ya 15 Bora ya Redd's Miss Tanzania.
Majaji wa shindano hilo walilazimika kumpa ushindi Prisca kutokana na uhodari wake wa kucheza na moto, hivyo kuwashinda washiriki wote 30 wa shindano hilo.
Watazamaji wengi waliofurika katika ukumbi wa hoteli hiyo, walikubaliana na uamuzi wa majaji wa kumpa ushindi huo.

Shindano la Redd's Miss Tanzania linatarajiwa kufanyika mwishoni mwa wiki katika Ukumbi wa Mlimani City, uliopo Mwenge, Dar es Salaam ambapo mshindi ataondoka na gari dogo lenye thamani ya sh milioni 15 na kitita taslimu cha fedha cha sh. milioni 8.
Mbali na mshindi kutwaa zawadi hizo, mshindi wa pili atapata sh. milioni 6.2, mshindi wa tatu sh. milioni 4, mshindi wa nne sh. milioni 3, mshindi wa tano sh. milioni 2, mshindi wa sita hadi 15 atapata sh. milioni 1.2 na waliobaki watapata sh. 700,000 kila mmoja.
Akizungumzia ushindi huo, Prisca alisema hiyo ni dalili njema kwake ya kutwaa taji hilo na ana uhakika mkubwa atafanikiwa kuwa mshindi.

Naye Meneja wa Redd's Original, Victoria Kimaro alisema, shindano la mwaka huu limekuwa na msisimko mkubwa zaidi kutokana na washiriki wote kuwa na sifa zinazolingana.
"Mwaka huu Redd's Miss Tanzania imepata washiriki bomba zaidi na naamini litakuwa na ushindani mkubwa na wa aina yake," alisema Victoria.

Taji la Redd's Miss Tanzania kwa sasa linashikiliwa na Brigitte Alfred aliyelitwaa taji hilo mwaka jana na kukabidhiwa gari aina ya Noah pamoja na kitita cha sh. milioni 8.
Shindano la Redd's Miss Tanzania linadhaminiwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia kinywaji chake cha Redd's Original.

No comments:

Post a Comment