Cristiano
Ronaldo ameifungia bao Real Madrid jana usiku na kuvunja rekodi ya
mmoja wa washambuliaji waliopo katika orodha ya kufunga mabao mengi
zaidi enzi zao wakisakata soka.
Mshambuliaji
huyo raia wa Ureno amefunga mabao 164 katika michezo 151 na kuvunja
rekodi ya mshambuliaji wa zamani wa Mexico, Hugo Sanchez aliyefunga
mabao 164 katika mechi 207.
Ronaldo
ameingia katika orodha ya wafungaji wanne wa juu waliowahi kufunga
mabao mengi katika historia ya Real, lakini amebakiwa na rekodi tatu
kuzivunja, yaani ya Santillana mwenye magoli 186, Alfredo Di Stefano
magoli 216 na Raul aliyetia kambani magoli 228.
Real
Madrid waliwafunga Valencia mabao 3-2 jana, shukurani zimwendee Ronaldo
kwa kichwa chake mahiri dakika ya 40 kufuatia mpira mzuri wa adhabu
uliochongwa na Agel Di Maria alimbadili Gareth Bale katika mchezo huo.
Madrid walipata bao la tatu na la ushindi kupitia kwa kinda wao mwenye miaka 20 Jese Rodriguez katika dakika ya 84.
Bao la kwanza lilifungwa na Angel Di Maria katika dakika ya 28 kufuatia kuwazidi ujanja mabeki wa Valencia.
Mabao ya Valencia yalifungwa na Pablo Piatti dakika ya 34 na Jérémy Mathieu dakika ya 62.
Kikosi
cha Valencia jana: Guita, Pereira, Ruiz, Mathieu, Romeu, Feghouli,
Bernat, Parejo (Banega, 84), Cartabia, Piatti (Guardado, 80), Jonas.
Kikosi
cha Real Madrid: Lopez, Arbeloa (Carvajal, 80), Ramos, Nacho, Marcelo,
Alonso, Modric, Di Maria (Illarramendi, 87), Isco (Jese, 73), Ronaldo,
Benzema.
Rekodi:
Bao la Cristiano Ronaldo jana usiku dhidi ya Valencia limemfanya
aungane na wafungaji wanne waliowahi kufunga mabao mengi katika historia
ya Real Madrid
Akiruka kwa furaha: Ronaldo aliifungia bao la pili Real Madrid katika ushindi wa mabao 3-2 jana usiku
Jitihada
ya timu: Ronaldo akipongezwa na wachezaji wenzake baada ya kufunga bao
la pili lililowafanya waende mapumziko wakiwa mbele kwa mabao 2-1
Kifua mbele: Angel di Maria na beki wa kushoto Marcelo wakishangilia bao la Margentina huyo
Amesawazisha: Mchezaji wa Valencia, Pablo Piatti (katikati) akishangilia na wachezaji wenzake baada ya kusawazisha bao
Kipute kinaendelea: Beki wa Valencia, Mfaransa , Jeremy Mathieu akishangilia baada ya kusawazisha bao la pili dakika ya 62
Mshindi: Mshambuliaji Jese (kushoto) akishangilia na mchezaji mwenzake Luka Modric baada ya kuifungia Madrid bao la ushindi
Aaaah! nimekosaje?: Beki wa Real Madrid, Sergio Ramos akishika kichwa chake baada ya kupoteza nafasi ya wazi kufunga bao
Changamoto: Kiungo wa Real Madrid , Xabi Alonso akimtoka winga wa Valencia Pablo Piatti katika mchezo wa jana usiku
No comments:
Post a Comment