Baadhi
ya vijana waliopata ufadhili wa kozi mbalimbali za ufundi toka Help for
Underserved Communities Inc. (HUC), wakisubiri taratibu za ujazaji fomu
za kujiunga katika Chuo cha Mafunzo ya Ufundi(VETA) jijini Dar es
salaam, hivi karibuni.
Monica
Mhelela na Fadhili Munda wakijaza fomu za kujiunga na kozi za ufundi
VETA jijini Dar es Salaam hivi karibuni. Vijana hao ni miongoni mwa
vijana wanaofadhiliwa na Help for Underserved Communities Inc. (HUC) |
Monica and Fadhili Munda fill application forms to attend training at
Vocational Education and Training Act (VETA) recently. These are among
11 youth who got scholarships from Help for Underserved Communities Inc.
(HUC).
Baadhi
ya vijana walipata ufadhili wa masomo ya ufundi toka Help for
Underserved Communities Inc. (HUC), wakijaza fomu za kozi mbalimbali
walizoomba VETA, jijini Dar es Salaam hivi karibuni. Kutoka kulia ni
Monica Mhelela, Joseph Mboya na Hassan Bakari.
Jamila
Mwenda na Joseph Mboya wa Dar es Salaam, wakionesha nyuso za furaha
baada ya ndoto zao za kusomea usekretari kwa Jamila na ufundi magari kwa
Joseph kutimia. Jamila na Joseph ni miongoni mwa vijana 11
wanaofadhiliwa na Help for Underserved Communities Inc. (HUC)
Vijana
11 waliopata ufadhili wa kozi mbali mbali VETA kupitia ufadhili wa Help
for Underserved Communities Inc. (HUC), yenye makao yake Marekani.
Picha zote na Nathan Mpangala. Zaidi: : https://www.facebook.com/pages/Help-for-Underserved-Communities-HUC-USA/412893725452394
Na Nathan Mpangala
Help
for Underserved Communities Inc. (HUC), imefadhili wanafunzi 11 kutoka
mikoa ya Dar es Salaam, Mbeya na Morogoro kozi mbalimbali za ufundi
zinazotolewa VETA, ambapo baadhi yao wameshaanza mafunzo na wengine
wanatarajiwa kuanza Januari mwakani.
Akizungumzia
ufadhili huo, Rais wa asasi hiyo, Bi. Zawadi Sakapalla – Ukondwa,
alisema, “ufadhili umelenga vijana wenye nia ya kujiendeleza lakini
wamekuwa wakishindwa kufanya hivyo kutokana na uyatima na wazazi au
walezi kutokuwa na uwezo wa kuwasomesha”.
Majina,
kozi na mikoa wanayotoka vijana hao ni; Joseph Mboya, Saidi Makope,
Yasini Musa (ufundi magari, Dar es Salaam), Neema Bungara (umeme wa
magari, Dar es salaam), Francis Mustafa (ufundi magari, Morogoro),
Hassan Bakari, Fadhili Munda (udereva, Dar es Salaam), David Mwasyeba
(udereva wa pikipiki, Mbeya), Jamila Mwenda (usekretari/kompyuta, Dar es
Salaam), Monica Mhelela (saluni na utengenezaji nywele, Dar es Salaam)
na Rose Mawawa (ufundi cherehani, Dar es Salaam).
HUC
ni asasi isiyo ya kiserikali yenye makao yake Marekani, inayosaidia
upatikanaji wa maji safi na salama ya kunywa, maktaba za kijamii na
vifaa vya elimu kwa maeneo yenye upungufu wa huduma za kujamii.
Habari zaidi: https://www.facebook.com/pages/Help-for-Underserved-Communities-HUC-USA/412893725452394
No comments:
Post a Comment