Mkurugenzi
wa shule ya kimataifa ya Southern Highlands Mafinga Bi Mary
Mungai akimkabidhi cheti mmoja kati ya wahitimu wa mahafali ya 13
shule hapo ,kulia kwake ni kaimu meneja wa Benk ya wananchi Mufindi
(Mucoba) Bw Ben Mahenge
Walimu
na wafanyakazi wa shule ya Southern Highlands Mafinga wakiwa katika
picha ya pamoja na mkurugenzi mtendaji wa shule hiyo Bi Mary Mungai
kushoto wa kwanza .
……………………………………………………….
Na Francis Godwin
MAENDELEO
mazuri ya ufaulu wa wanafunzi wa shule ya kimataifa ya Southern
Highlands Mafinga mkoani Iringa iliyoisukuma benk ya wananchi Mufindi
(MUCOBA) kujitokeza kuunga mkono jitihada za elimu katika shule hiyo .
Ifahamike kuwa suala
la motisha kwa walimu na wanafunzi wanaofanya vema katika
masomo yao na walimu wanaofundisha wanafunzi hao ni moja na
hamasa kubwa kwa kuwawezesha kufanya vizuri katika
maendeleo ya elimu nchini.
Yamekuwepo malalamiko mbali mbali kutoka
kwa wadau wa elimu nchini ambao wamekuwa wakilalamikia maendeleo
mabaya ya elimu nchini hasa kutokana na mazingira
duni ya kufundishia malalamiko ambayo serikali kupitia wizara
ya elimu na mafunzo ya ufundi imeendelea kuyafanyia kazi
Huku wale waliokuwa wakibeza shule za
kata hivi sasa kuanza kuzipongeza shule hizo kutokana na baadhi
ya shule hizo kufanya vizuri kuliko shule za
awali ambazo walikuwa wakizisifia na hapa ndipo tunaungana
na wahenga waliosema kupanga ni kuchagua .
Pia miaka ya hivi karibuni zimezuka shule nyingi za
sekondari na msingi za watu binafsi ambazo
baadhi ya shule hizo zimeendelea kufanya vizuri
na kutoa changamoto kubwa kwa shule za serikali na baadhi ya
shule zilizoanzishwa na watu binafsi zikionekana kuendelea kushuka
zaidi na wazazi hata kuamua kuhamisha watoto wao.
Shule
ya Southern Highlands Mafinga imeonekana kuivutia zaidi benki hiyo ya
MUCOBA kutokana na rekodi yake nzuri ya kufaulisha vizuri wanafunzi
wote darasa la saba tangu ilipoanzishwa mwaka 1997.
Kiwango cha elimu kinachotolewa
katika shule ya kimataifa ya Southern Highlands Mafinga kinaisukuma
benk ya wananchi wilaya ya Mufindi (MUCOBA) kuahidi kutoa kiasi
cha Tsh milioni 2.5 kwa ajili ya kuwafuingulia akaunti katika benk
hiyo wanafunzi waliofanya vema matokeo ya mtihani huo mwaka
huu.
Bw
Ben Mahenge anasema kuwa moja kati ya sababu iliyopelekea benki
yake kujitokeza kuunga mkono jitihada za shule hiyo ni kutokana
na ufaulu mzuri wa mitihani ya Taifa ya darasa la saba ambayo
shule hiyo imeendelea kuongoza na hivyo kutoa heshima kwa wilaya
ya Mufindi na Tanzania kwa ujumla.
Kwani
anasema kuwa mbali ya benk hiyo kuendelea kutoa mikopo mbali
mbali ila imekuwa karibu zaidi na shule hiyo ya Southern Highlands
Mafinga ambapo mkurugenzi wake Bi Mary A. Mungai ni mmoja kati ya
wateja wakubwa wa benk hiyo kutokana na
wazazi
wote wanaosomesha watoto katika shule hiyo kulipia ada kupitia
benk hiyo hivyo kiasi hicho cha fedha kilichotolewa na MUCOBA ni
kutambua mchango wa shule hiyo katika uendelezaji wa benk hiyo.
”
Kati ya wateja wakubwa wa benk ya MUCOBA ni pamoja na shule ya
Southern Highlands Mafinga na wazazi ambao wanasomesha watoto hapo
kutokana na wazazi wa watoto wanaosomesha hapo hulipa ada kupitia
benk yetu …..hivyo kwa ajili ya kumpongeza mkurugenzi wa shule
hiyo kwa kuzidi kuiunga mkono benk yetu bado tunazidi
kuwahamasisha wananchi wa wilaya ya Mufindi na nje ya mkoa wa
Iringa kujiunga nasi”
Mahenge
anasema kuwa benk hiyo imeendelea kutoa mikopo mbali mbali kwa
wateja wake ikiwemo mikopo ya ujenzi wa nyumba bora , ujasiliamali
na mikopo ya kuendeshea biashara .
Hata
hivyo Mahenge anasema kuwa wanafunzi watakaonufaika na msaada
huo ni yule aliyefanya vizuri katika matokeo ya mtihami wa
Taifa wa darasa la saba pamoja na mwanafunzi Aida Mhagama ambae
aliibuka mshindi wa jumla katika masomo mbali mbali na kupongezwa
wakati wa mahafali ya darasa la saba ya shule hiyo .
Anasema
fedha hizo zitaingizwa katika akaunti zao baada ya kufunguliwa na
benk hiyo kwa lengo la kusaidia kuwasomesha elimu ya sekondari
pindi watakaojiunga na elimu hiyo ya sekondari mapema mwakani .
Mkurugenzi
mtendaji wa shule hiyo Bi Mary Mungai ambae amepata kuwa
afisa elimu shule za msingi anasema kuwa shule imekuwa ikifundisha
kwa kiingereze, yaani english medium school, imefaulisha tena mwaka huu
2013 wahitimu wote wa darasa la saba na kuiwezesha kuwa katika asilimia
mbili (2%) ya juu ya shule zote zenye kufaulisha vizuri kitaifa, na
katika 10 bora kati ya shule 449 za mkoani Iringa.
“…Tunawapa
hongera wahitimu hao na kuwatakia maendeleo mazuri kokote waendako.
….pia tunawapongeza wazazi/walezi, tunawatakia kila la heri kuwaendeleza
watoto wao kufuatia msingi huu ulio bora waliopata kutoka Southern
Highlands School.
Anasema
pia uongozi wa shule hiyo hautaacha kuwapongeza walimu, kwa kazi
kubwa wanayoendelea kuifanya kila siku kuhakikisha wanafunzi wanapata
elimu iliyo ya kiwango cha juu.
“
Sisi tunapokea watoto kutoka pande zote za nchi na
watakaotaka watoto wao wajiunge na Southern Highlands School, nafasi
zipo kwa wanafunzi wa chekechea, darasa la 1, 2, 3, na 5 kwa wanafunzi
wote na darasa la 4 na la 6 kwa wanaotoka shule za English Medium
Anasema kuwa toka shule hiyo ilipoanzishwa mwaka 1994 kama Day Care na Pre-school na mwaka 1997 kuanza shule ya msingi imekuwa ikifanya vizuri na hakuna mtoto aliyepata kufeli .
“Shule yetu
mwaka 2001 shule ilitoa wanafunzi wa kwanza wa darasa la Saba na
wanafunzi walikuwa 17, wote walifaulu vizuri na wote walichaguliwa
kuendelea na masomo ya kidato cha kwanza”
Anasema katika matokeo
ya mitihani ya darasa la 7 ya mwaka 2001 Southern Highlands School
ilishika nafasi ya kwanza kitaifa katika mitihani ya Somo la Kiingereza.
“
Tulimshukuru Mungu na tunaendelea kumshukuru Yeye. Kwa kuwezesha watoto
wetu wa Southern Highlands School, kufaulu vizuri, kwa kishindo”
alisema Bi Mungai
Hata hivyo anasema kila mwaka wanafunzi wote wamekuwa wakifaulu mitihani ya kitaifa ya darasa la saba na wote kuchaguliwa na kuendelea na masomo ya Sekondari.
“mwaka huu
tena wanafunzi wote wa darasa la saba 47 waliomaliza mwaka huu 2013,
wamefaulu na kuchaguliwa kuendelea na sekondari”
Mwenyekiti wa bodi ya shule hiyo Bw Omary Mahinya anasema kuwa katika moja ya vielelezo kuwa shule hiyo ni bora nchini ni wazazi kutoka mikoa karibu yote ya Tanzania kupeleka watoto wao hapo .
No comments:
Post a Comment