Baadhi
ya wachezaji wa timu ya Taifa wa ngumi za Ridhaa pamoja na wadau
wengine wa mchezo huo katika Picha ya pamoja, wakati wa hafra hiyo
Aliyesimama
kushoto ni mkurugenzi wa Afrika Mashariki kupitia kinywaji cha Battery
Bwana Tony Misokia akiwa anaongea na wananchi walioshiriki katika Hafra
hiyo.
Kutoka
kushoto ni Makamu wa Rais wa Shirikisho la Ngumi za ridhaa Tanzania
(BTF) Bwana. Lukelo Anderson akiwa sambamba na Afisa habari wa Ngumi za
ridhaa Tanzania Bwana Salum Viduka wakati wa Hafla hiyo.
Hawa ni Baadhi ya wachezaji wa Shirikisho la Ngumi za ridhaa Tanzania (BTF)
Wa kwanza kulia ni Nahodha wa Timu ya Taifa ya Ngumi za ridhaa Tanzania bwana Nassari Mafuru
Kutoka
kushoto aliyevaa shati jeupe ni Bwana Anthon Mwang’onda ambaye ni
mjumbe wa mashindano na vifaa wa Shirikisho la Ngumi za ridhaa Tanzania
(BTF) akiwa na Kocha Mkuu wa timu ya Taifa Bwana Hassan Mzonge
Shirikisho
la ngumi za ridhaa Tanzania limefanya hafla fupi iliyojumuisha
wachezaji wa ndondi , makocha wadau na Vyombo vya habari kwaajili ya
kuendeleza mshikamano wa kuweza kuwainua vijana ambao bado
hawajaweza kupata ajira kujiunga na shilikisho la ngumi za ridhaa Tanzania
hawajaweza kupata ajira kujiunga na shilikisho la ngumi za ridhaa Tanzania
Shilikisho
hilo ambalo limeanzisha mashindano ambayo yanatambulika kwa jina la
PSPF Boxing Award sambamba na wadhamini wa mashindano hayo waliandaa
hafla hiyo iliyofanyika katika eneo la (CnG) ambapo waliweza
kudhamini kwa kuandaa chakula cha usiku kwaajili ya kuendelea kuweka
mahusiano baina ya washiriki wote wanao shiriki katika kuendeleza mchezo
wa ngumi Tanzania
Akizungumzia
lengo la kuweka hafla hiyo Afisa habari wa shirikisho la ngumi
Tanzania Bw.Salum Kuhowa Viduka amesema “Tunawaomba wanajamii kuweza
kutupa ushirikiano kwa muda wote ambao mashindano haya huwasili katika
miji,wilaya, manispaa, nk kuweza kujitokeza kwa wingi ili kuona jinsi
fursa kwa vijana zinavyo patikana kupitia mchezo wa ngumi za Ridhaa”
Mwisho
Makamu Rais Bw.Lukelo Andason aliweza kufunga hafla hiyo kwa
kuwapongeza watu wote walio weza kufika na kujumuika pamoja ili
kuendeleza kujenga umoja wa ngumi Tanzania.
No comments:
Post a Comment