KLABU
ya Kagera Sugar inaingia kambini desemba 31 mwaka huu, lakini mazoezi
yataanza rasmi januari pili mwakani kujiwinda na mzunguko wa pili ligi
kuu soka Tanzania bara unaotarajia kuanza kushika kasi januari 25, 2014.
Kocha msaidizi wa klabu hiyo, Murage Kabange ameuambia mtandao huu kuwa nia yao ni kurejesha makali yao kama msimu uliopita.
“Mipango
ya kambi imekamilika, mimi na kocha mkuu Jackson Mayanja tunajiandaa
kukisuka kikosi chetu upya. Kuna makosa yaliyokuwepo mzunguko wa kwanza,
tuliyagundua mapema na sasa kazi ni kurekebisha tu”. Alisema Kabange..
Kabange
aliongeza kuwa katika dirisha dogo la usajili wamemuongeza Andrew
Mathew kazembe kutoka Abajalo FC ili kukamilisha idadi ya wachezaji 25.
“Tulitumia
muda mrefu kumchunguza mchezaji huyo, tumezingatia nidhamu na uwezo
wake, kwa kiasi kikubwa atatusaidia ngwe ya pili ya ligi kuu bara”.
Aliongeza Kabange.
Aidha
kocha huyo alisema tatizo la safu ya ulinzi limepata dawa baada ya beki
wao wa kati, Amandus Nestar kurejea uwanjani kufuatia kupoma tatizo
lake la mguu.
“Karibu
mzunguko mzima, Nestar amekuwa akisumbuliwa na mguu, madaktari
wamefanya jitihada kubwa kuhakikisha anarejea uwanjani. Hivi
ninavyozungumza na wewe, beki huyo yuko tayari kuanza mazoezi na hali
hii itaimarisha safu yetu ya ulinzi”. Alisema Kabange.
Kwa
upande wake mshambuliaji hatari wa Kagera Sugar, Them Felix alisema kuwa
anajiandaa vikali kuhakikisha anaisadia klabu yake kufanya vizuri na
hatimaye kuingia tatu bora msimu huu.
Them
aliongeza kuwa mchezaji wa mpira wa miguu hana mapumziko, pale timu
inapopewa mapumziko, yeye anatakiwa kutafuta njia mbadala ya kufanya
mazoezi binafsi ili kulinda uwezo wake na kasi yake.
“Binafsi
nimekuwa nikifanya mazoezi na Bukoba Veteran, nimejijanga vizuri na
nina uhakika wa kufanya vizuri. Kikubwa Mwenyezi Mungu atupe afya
njema”. Alisema Them.
Msimu
wa mwaka jana, Kagera Sugar ikiwa chini ya kocha Mkongwe, Alhaji
Abdallah Athuman Seif `King Kibadeni Mputa` ilishika nafasi ya nne
katika msimamo wa ligi kuu, huku nafasi ya tatu ikishikwa na Simba, ya
pili Azam fc na mabingwa walikuwa Dar Young Africans.
Msimu
wa mwaka huu, klabu hii haijawa na matokeo mazuri sana kwani mpaka
mzunguko wa kwanza unamalizika, tayari imeshajikusanyia pointi 20 katika
nafasi ya sita.
No comments:
Post a Comment