RC Iringa Dr Christine Ishengoma
Mkuu
wa mkoa wa Iringa Dr Christine Ishengoma ametuma salama kali za
Krismas na Mwaka mpya kwa wafanyabiashara watakaopandisha bei ya
vyakula msimu huu wa sikukuu kuwa watachukulia hatua kali.
Huku
akiwataka wakurugenzi wa Halmashauri zote za wilaya ,wakuu wa wilaya
,maofisa biashara wa wilaya na mkoa huo kuanza kuzunguka mitaani
kuchunguza bei ya bidhaa na kuwataka kuchukua hatua kwa wote
wanaliopandisha bei kiholela.
Akizungumza
na wanahabari jana ofisini kwake ,mkuu huyo wa mkoa alisema kuwa
imekuwa ni kawaida kwa baadhi ya wafanyabiashara kutumia sikukuu
mbali mbali kujipatia fedha kwa kuwanyonya wananchi jambo ambalo
katika mkoa huo halitavumiliwa kamwe.
Alisema
kuwa lengo la serikali ya mkoa kuwabana wafanyabiashara ni
kutaka kuona wananchi wanasherekea sikukuu hizo na kununua
vyakula na vitu mbali mbali vya sikukuu kulingana na bejeti
waliyoitenga kwa sikukuu hizo.
”
Serikali ya mkoa haitakubali kuona wananchi wakiibiwa kwa kuuziwa
vyakula kwa bei kubwa za sikukuu….tumejipanga kuchukua hatua kali
na tunaomba wananchi pia kutoa ushirikiano “
Hata
hivyo mkuu huyo wa mkoa alivipongeza vyomba vya habari mkoani
Iringa kwa mchango mkubwa wa kuhamasisha maendeleo na kutaka
kuonyesha ushirikiano katika wakati huu wa sikukuu kwa kufanya
uchunguzi wa wafanyabiashara wanaopandisha bei.
Katika hatu nyingine mkuu huyo wa mkoa aliwataka wakulima kutumia mvua zinazoendelea kunyesha kwa kupanda mazao mbali mbali yakiwemo yale yanayohimili ukame kwa maeneo yeye changamoto ya mvua.
Katika hatu nyingine mkuu huyo wa mkoa aliwataka wakulima kutumia mvua zinazoendelea kunyesha kwa kupanda mazao mbali mbali yakiwemo yale yanayohimili ukame kwa maeneo yeye changamoto ya mvua.
Pia
aliwataka maofisi kilimo na mabwana shamba kuachana na mpango wa
kuvaa suti na kushinda maofisini wakati huu wa msimu wa kilimo badala
ya kwenda kuwaelimisha wakulima .
Dr
Ishengoma aliwataka wakulima kuendelea kutumia mbolea ya Minjingu
ambayo alidai hata yeye amekuwa akiitumia na ni miongoni mwa mbolea
bora nchini na kuwataka kuepuka maneno ya kukatisha tamaa
yanayoendelea kutolewa na watu juu ya mbolea hiyo.
Wakati
huo huo serikali ya mkoa wa Iringa imepiga marufuku wazazi
kuwaruhusu watoto wao kwenda kushiriki madisco toto ambayo alidai ni
hatari na ni vema wazazi na walezi wa watoto mkoani Iringa kuwa
makini na kuachana na tabia ya kuwaacha watoto wao peke yao wakati
huu wa sikukuu.
No comments:
Post a Comment