Manchester
United wametoka nyuma kwa mabao 2-o na kuibuka na ushindi wa mabao 3-2
dhidi ya Hull City katika dimba la KC, huku shukurani za pekee
zikimwendea mchezaji wa zamani wa mashetani wekundu, James Chester
aliyejifunga bao la tatu na kuizamisha klabu yake ikiwa nyumbani.
Hata
hivyo James Chester ndiye aliyekuwa wa kwanza kuiandikia kimiani bao la
kwanza klabu yake ya Hull dakika ya nne tu ya mchezo huo baada ya kazi
nzuri ya Alex Bruce.
David
Meyler katika dakika ya 13 aliandika bao la pili kufuatia makosa ya
mabeki wa Man United, lakini mashetani wekundu walikuja juu na katika
dakika ya 25 Chris Smalling alifunga bao zuri kwa njia ya kichwa
akimalizia kazi nzuri ya Wayne Mark Rooney.
Dakika moja tu baadaye, Rooney alitinga tena nyavuni na kusawazisha bao la pili.
Man
United walimaliza kazi katika dakika ya 646 baada ya James Chester
kujifunga mwenyewe akiunganisha mpira wa krosi wa Ashley Young na kumpa
ushindi wa bure David Moyes.
Muda wa shangwe: Man United wamesogea mbele baada ya ushindi wa leo
Tumemaliza?: Wachezaji wa Man United wakishangilia bao lao la tatu ambalo Hull walijifunga kutokana na krosi ya Ashley Young
Mikoni kichwani, umeharibu baba!: James Chester akijifunga bao na kuizamisha Hull leo dhidi ya Man United
David Moyes amepumua
Mchezo unaoendelea kwa sasa ni
baina ya Manchester City dhidi ya Liverpool katika dimba la Etihad, na
mpaka dakika ya 30, Majogoo wako mbele kwa bao moja lilolofungwa
na Philippe Coutinho
MATOKEO YA MECHI ZILIZOMALIZIKA;
England: Premier League
Finished
|
|
2-3 |
Manchester United
|
(2-2) | ||||||
Finished
|
|
1-1 |
West Bromwich Albion
|
(1-1) | ||||||
Finished
|
|
1-2 |
Fulham
|
(1-1) | ||||||
Finished
|
|
5-1 |
Stoke
|
(1-1) | ||||||
Finished
|
|
1-3 |
Arsenal
|
(0-0) | ||||||
Finished
|
|
0-1 |
Sunderland
|
(0-1) | ||||||
Finished
|
|
1-0 |
Swansea
|
(1-0) | ||||||
Finished
|
|
0-3 |
Southampton
|
(0-3) | ||||||
Finished
|
|
0-1 |
Crystal Palace
|
(0-0) | ||||||
30′
|
|
0-1 |
Liverpool
|
No comments:
Post a Comment