Na Mwandishi Wetu
WAZIRI
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Uratibu na Bunge, William Lukuvi
anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika Tamasha la Krismasi Uwanja wa Taifa
Dar es Salaam, Desemba 25 mwaka huu.
Taarifa
kwa vyombo vya habari iliyotolewa Dar es Salaam jana na Mwenyekiti wa
Kamati ya Maandalizi ya tamasha hilo, Alex Msama ilieleza kuwa
maandalizi kuhusiana na tamasha hilo yanaenda vizuri.
“Hamasa
imekuwa kubwa pengine kuliko matamasha mengine ambayo Kampuni yangu ya
Msama Promotions imewahi kuyaandaa. Waimbaji wanatamani siku ifike
wafanye mambo, mashabiki nao wanatamani siku ifike waone mambo.
“Pia
nafurahi kuwajulisha kuwa Waziri Lukuvi amekubali kuwa mgeni rasmi
Desemba 25 Uwanja wa Taifa Dar es Salaam, naamini siku hiyo itakuwa
burudani ya aina yake. Namshukuru sana kwa kuungana nasi,” alisema
Msama, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi Tamasha la
Pasaka.
Alisema
kiingilio cha chini katika tamasha hilo kwa upande wa Uwanja wa Taifa
kitakuwa sh. 5000 na viingilio vingine vitakuwa sh 10,000 na sh.20,000
kwa majukwaa maalum A na B.
“Pia
watoto watachangia sh. 2,000, tumeweka viingilio vya kawaida ili wote
tuweze kuhudhuria Uwanja wa Taifa,” alisema Msama na kuongeza kuwa kwa
mikoani viingilio ni sh 5,000 kwa wakubwa na watoto itakuwa Sh 2,000.
Waandaaji
hao wamepanga tamasha hilo lifanyike Desemba 25 Uwanja wa Taifa, Dar es
Salaam na siku inayofuata Uwanja wa Jamhuri, Morogoro, kisha Desemba 28
Uwanja wa Mkwakwani Tanga na Desemba 29 Uwanja wa Sheikh Amri Abeid,
Arusha.
No comments:
Post a Comment