Mwakilishi wa Mitandao ya Kijamii nchini (CCT), Jennifa Chiwute |
Watoto
yatima nchini wako hatarini kufanyiwa vitendo vya ukatili wa kijinsia
ilikinganishwa na kundi la wanawake, watoto na watu wenye ulemavu.
Akizungumza
jana katika mdahalo ulioandaliwa na mtandao wa kupinga ukatili wa
kijinsia (MKUKI) ulioratibiwa na Shirika la Kupinga Ukatili wa Kijinsia
Tanzania (AFNET)Kanda ya Kati uliofanyika mjini hapa, Mwakilishi wa
Mitandao ya Kijamii nchini (CCT), Jennifa Chiwute, alisema taarifa ya
Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) kwa mwaka 2009
kuhusiana na vitendo vya ukatili wa kijinsia nchini, imeonyesha kundi
hilo la watoto yatima liko kwenye hatari zaidi ya kufanyiwa vitendo
hivyo kwa kuwa wengi wao hawana ulinzi kutoka kwa mtu yeyote.
Akiwasilisha
mada kuhusiana na mpango wa kukomesha vitendo hivyo, Chiwute, alisema
taarifa hiyo ilionyesha kuwa asilimia 30 ya wasichana na asilimia 14.3
ya wavulana, waliwahi kutendewa kitendo kimoja cha ukatili wa kijinsia
kabla ya kufikisha umri wa miaka 18 huku asilimia 60 ya wasichana
walilazimishwa kujamiina.
Alibainisha
pia inaonyesha kuwa wasichana hao walilazimishwa kujamiiana na ndugu,
jirani, marafiki na watu wasiowafahamu wenye umri mkubwa.
“Waathirika
wenyewe wanafanyiwa kwenye maeneo ya nyumbani kwa mtu, shuleni au
njiani wakati wa kwenda au wa kurudi shuleni,” alisema Chiwute.
Alisema vitendo hivyo ni pamoja na ukatili wa kipigo, ukeketaji, kingono na kiakili.
Alisema vitendo hivyo ni pamoja na ukatili wa kipigo, ukeketaji, kingono na kiakili.
Alionya
kuwa iwapo vyombo vya dola havitachukua hatua za kisheria kwa
wanaotenda vitendo hivyo, hali itazidi kuwa mbaya zaidi kwa siku zijazo.
“Vyombo
vya serikali vimeshindwa kusimamia kwa dhati utekelezaji wa sheria
zinazolinda haki za wanawake, watoto na watu wenye ulemavu kwa sababu ya
rushwa,”alisema Chiwute.
Kwa
upande wake, Mkurugenzi wa AFNET Tanzania, Sarah Mwaga, alisema ni
wajibu wa wadau wote na watetezi wa haki za binadamu kuungana kukomesha
vitendo vya ukatili wa kijinsia ambavyo vina madhara makubwa kwa
watendewa.
Naye
Mkuu wa Kitengo cha Dawati la Jinsia Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma,
Hamida Hiki, alisema kuwa jeshi hilo linakabiliwa na changamoto ya jamii
kuwa na mfumo dume ambao ndiyo chanzo cha vitendo vya ukatili ambavyo
vinasababisha wimbi la watoto wa mazingira hatarishi mitaani.
No comments:
Post a Comment