Na Mussa Mkama
MKURUGENZI
Mtendaji wa Msama Promitions Alex Msama amekabidhi msaada wa magodoro
yenye dhamani ya zaidi ya Shilingi milioni 4 kwa kituo cha watoto yatima
Luhila Pachane kilichopo Songea Mkoani Ruvuma.
Alex Msama |
Akizungumza
na waandishi wa habari katika makao makuu ya ofisi za Msama Promotions
Kinondoni Jijini Dar es Salaam jana Msama alisema msaada huo umetoka
kwenye mfuko wa Tamasha la Krismas ambalo linatarajiwa kuanza Desemba 25
jijini hapa na mikoa mingine.
Tamasha hilo la Krismas linatarajia kufanyika katika mikoa mitano, ambapo ni Dar es Salaam, Morogoro, Tanga, Arusha na Dodoma.
Msama
alisema kuwa kutokana na maombi ya kituo hicho na kuguswa na hali
waliyokuwa nayo ya yatima hao kulala katika mkeka, aliamua kunyofoa
sehemu ya fedha zilizokuwa kwenye mfuko wa Tamasha la Krismas na kuamuo
kuwasaidi watoto hao ili nao waweze kujisikia wapo katika jamii ya
Watanzania.
“Nimeamua
kufanya hivyo kutokana na kuguswa na hali halisi waliyonayo yatima hao
wa kituo cha Luhila Pachane huko mkoani Ruvuma nikaamua kunyofoa fedha
katika mfuko wa Tamasha la Krismas kwa ajili ya kuwasaidi ili nao
wajisikie wako pamoja na Watanzania wenzao” alisema Msama na kuongeza
kuwa;
“Msaada
huo wa magodoro hayo ni zaidi ya shilingi milioni 4, hivyo ninaimani
kubwa sasa kwa msaada huu yatima wataniombea kwa Mungu ili Tamasha la
Krismas liwe la mafanikio kwani lengo la tamasha hilo ni kuweza kujenga
kituo cha kisasa cha watoto yatima na wasiojiweza kwani kiwanja
tumeshakiona kipo pale maeneo ya barabara ya Pugu Jijini Dar es Salaam.
Akizungumza
baada ya kukabidhiwa msaada huo Mlezi wa kituo hicho ambaye pia ni
Katibu wa Bakwata mkoa wa Ruvuma Shekh Abdushakur Omary alisema
anamshukuru Msama kwa wema wake aliouonyesha wa kusaidia jamii ya
Watanzania wote bila kubagua dini, kabila wala rangi.
“Msama
ni mtu wa aina yake hana ubaguzi anashughulikia maombi ya Watanzania
wote bila kuangalia dini, kabila, rangi wala utaifa wake kwani amaamini
kuwa wote ni wamoja, hivyo naomba nizidi kumuombea aendelee kuwa na moyo
huo wa kujitolea kwa ajili ya watu wa taifa lake wasiyojiweza” alisema
Omary.
Hata
hivyo aliomba Wizara husika kuharakisha upatikanaji wa hati ya kiwanja
kile kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha kisasa cha kutolea misaada
(Center) pamoja na kiwanda cha kisasa cha kuzalishia kazi za wasanii
kwa manufaa ya Taifa na watu wake, kwani kwa kufanya hivyo itakuwa
imesaidia Watanzania wengi wenye ndoto ya kuwa wasanii wakubwa nchini.
“Uwepo
wa Msama katika ulimwengu huu kunamuwakilisha Mwenye Mungu, kwani Mungu
si mbaguzi kwa watu wake anawapenda wote na anatoa sawa kwa kila mtu,
hivyo ndivyo alivyo Msama, kwa moyo mmoja namuombea yeye na taasisi yake
isiyokuwa na ubaguzi wa dini kuendelea kuwa hivyo wakati wote” alisema
Omari na kuongeza kuwa;
“Naomba
Wizara au Waziri husika kuona umuhimu wa ujenzi wa kituo hicho cha
kisasa cha kutolea misaada pamoja na kiwanda cha kuzalishia kazi za wasanii,
kwani wapo Watanzania wengi wenye vipaji lakini hushindwa kufanya kazi
za kisanii kutokana na viwanda kuwa na gharama kubwa wasizoweza
kuzimudu”
No comments:
Post a Comment