Dar es Salaam. Wawekezaji wa Sekta ya miliki ya nyumba, wameunda umoja wao kwa kushirikiana na Shirika la Nyumba la Taifa(NHC).
Akitoa
ufafanuzi kuhusu hatua ya kuanzisha umoja huo uliopewa jina la Chama
cha Waendelezaji Miliki Tanzania, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba,
(NHC), Nehemia Mchechu alisema kuwa huo ni mwanzo wa safari ya kuwa na
muungano wa wawekezaji katika sekta hiyo wakishirikiana na Serikali.
Mchechu alisema wameanza na wawekezaji wakubwa 30, ambapo kadri siku zinavyokwenda anayetaka kujiunga atafanya hivyo.
Alisema
umuhimu wa kuwa na muungano huo ni kuweza kuishauri Serikali kujenga
kwa viwango badala ilivyo sasa kila mmoja anafanya kivyake.
Aidha,
Mchechu alisema kuwa Tanzania wamechelewa kuanzisha umoja huo kwani
mataifa mengi yameshafanya hivyo na kuzitolea mfano nchi za Kenya,
Uganda, Afrika ya Kusini na baadhi ya nchi Ulaya.
“Kwa
umoja huu tutajenga imani kwa wateja wetu, ambao watakuwa na sehemu ya
kukimbilia wanapoona mambo yanakwenda kinyume na matarajio,” alisema
Mchechu.
Naye
Mohamed Sharifu, Mtanzania anayeishi Dubai alisema kuwa amefurahishwa
na hatua hiyo kwa kuwa itapunguza idadi ya majengo mabovu.
No comments:
Post a Comment