Waziri
wa Ujenzi, John Magufuli akisisitiza jambo alipokuwa akikagua ujenzi wa
barabara, amewaonya makandarasi wasiofuta vigezo katika ujenzi wa
barabara nchini kwamba hatasita kuwatimua
Dar es Salaam.
Waziri wa Ujenzi, John Magufuli amewaonya makandarasi waliopewa kazi ya
ujenzi wa barabara kwenye Mikoa ya Dodoma, Manyara na Mtwara kutekeleza
yaliyomo kwenye mkataba vinginevyo hatasita kuwashughulikia.
Magufuli
aliyasema hayo jana kwenye hafla ya utiaji wa saini ujenzi wa barabara
kwenye mikoa hiyo uliofanywa na Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads)
na kampuni za ujenzi na usimamizi kutoka China na Ujerumani wenye jumla
ya Sh 539 bilioni.
“Kama
mnaona hamtatekeleza yaliyomo kwenye mkataba kama vile ujenzi kuchelewa
na kujenga chini ya kiwango, tafadhali msisaini mkataba huu kwa sababu
mtapata shida,” alisema.
Magufuli
alisema fedha za ujenzi wa barabara hizo ni mkopo kutoka Benki ya
Maendeleo ya Afrika (AfDB) ambao wametoa asilimia 65 ya kiasi hicho na
Wakala wa Ushiriano wa Kimataifa wa Japan (Jica) waliotoa asilimia 29
wakati serikali imetoa asilimia tano.
Aliwaagiza
watendaji wakuu wa Tanroads waliopo kwenye mikoa ya miradi hiyo
kusimamia ipasavyo ujenzi wa barabara hizo vinginevyo watahesabika kama
wameshindwa kazi. Aidha, Magufuli aliwataka Tanroads kufuata sheria
kuwashughulikia wenye malori wanaozidisha uzito kwani hao ndiyo
wanaosababisha uharibifu wa barabara zinazojengwa kwa gharama kubwa.
Miradi iliyosainiwa jana
Mtendaji
Mkuu wa Tanroads, Patrick Mfugale alisema mradi wa ujenzi wa kati ya
Mayamaya hadi Meela ambazo ni kilometa 99.35 mkoani Dodoma itajengwa na
kampuni ya China Henan International Cooperation Group kwa gharama ya Sh
100.1 bilioni.
Alisema kazi ya usimamizi wa mradi huo imepewa kampuni ya Crown Tech-Consult Ltd ya Tanzania kwa gharama ya Sh2.7 bilioni.
Alisema
mkataba wa ujenzi wa barabara kati ya Meela hadi Bonga kwa upande wenye
kilomita 88.8 umesainiwa na Kampuni ya China Railways Seventh Group Co.
Ltd kwa gharama ya Sh88.3 bilioni tekelezaji ni miezi 36 kuanzia jana.
“Usimamizi
wa mradi huo imepewa kampuni ya HP Gauff Inginieure GMBH na KG-JBG ya
Ujerumani kwa gharama za Euro 2, 357,200 sawa na Sh 4.9 bilioni.
Mfugale
alisema mkataba wa ujenzi kati ya Mangaka hadi Mtambaswala mkoani
Mtwara ambazo ni kilometa 65.5 imepewa Kampuni ya Sichuan Road and
Bridge Group Cooperation Ltd ya China.
Alisema kampuni hiyo itajenga kipande hicho kwa gharama ya Sh 60 bilioni na kwamba utekelezaji wake ni miezi 24.
Mfugale
alisema zabuni za ujenzi wa barabara hizo zilitangazwa Novemba Mosi,
2012 na kwamba kampuni 187 zilijitokeza kuomba kazi hiyo.
CHANZO: MWANANCHI
No comments:
Post a Comment