Wagonjwa watano wenye maradhi mbalimbali ya moyo wamekwenda nchini India kwa matibabu ambapo wengine watafanyiwa upasuaji.
Wagonjwa
hao ambao wanatarajiwa kurejea nchini baada ya wiki nne, wamefadhiliwa
kwa pamoja na Hospitali ya Regency Medical Center, Lions Club ya Dar es
Salaam (Host), Lions club ya Arusha na Prime Bank ya Kenya.
Shughuli
ya kuwaaga wagonjwa hao ilifanyika juzi jioni katika Uwanja wa Ndege wa
Kimataifa wa Julius Nyerere ambapo ilihudhuriwa na Rais wa Lions,
Nureen Nathoo, Rais wa zamani wa Lions, Shiraz Rashid, Mwenyekiti wa
kanda wa Lions, Lion Bakary Omary na mratibu wa maradhi ya moyo katika
klabu ya Lions, Dk. Rajni Kanabar.
Kwa
mujibu wa Dk. Kanabar, wagonjwa hao watatibiwa katika hospitali ya CIMS
iliyoko mji wa Ahmedabad nchini India kwa punguzo ya gharama ya Dola
2,500 za Marekani.
“Tunawashukuru
wasamaria wema wote waliofanikisha shughuli hii ikiwemo benki ya Kenya
ambayo imetoa dola 5,000 kwenye mradi wa kupeleka wagonjwa nje,”
alisema.
Dk.
Kanabar alisema fedha hizo zitatumika katika upasuaji wa mgonjwa mmoja,
tiketi na Dola 200 zitatolewa kwa wagonjwa wote ili ziwasaidie katika
maisha wakiwa ugenini.
Dk.
Kanabar alisema tangu kuanzishwa kwa mradi huo, watoto zaidi ya 2,500,
vijana na watu wazima wamepelekwa nje kwa ajili ya matibabu ya moyo.
Gilda
Sangwe, ambaye mtoto wake ana tundu kwenye moyo, aliwahsukuru watu
waliojiotolea fedha kwa ajili ya wagonjwa hao kwani bila hivyo
wasingemudu gharama.
CHANZO: NIPASHE
No comments:
Post a Comment