Jembe
la kazi la zamani la Simba Sc: Emmanuel Anord Okwi, leo hii amefunga
mawili katika mchezo muhimu wa CECAFA dhidi ya Eritrea na kupanda
kileleni mwa kundi C
……………………………………………………………………………
Na Baraka Mpenja
MECHI
za kundi C za kombe la Mataifa ya Afrika mashariki na kati, CECAFA
Challenge, zimeendelea leo ambao Mabingwa watetezi wa kombe hilo, Timu
ya Taifa ya Uganda imejihakikisha kutinga robo fainali baada ya kuifumua
Eritrea mabao 3-0, Uwanja wa City, jijini Nairobi, Kenya.
Mabao
ya Uganda leo hii yalifungwa na nyota wa zamani wa wekundu wa Msimbazi
Simba Sc, Emmanuel Anord Okwi aliyepiga mawili katika dakika ya 9 na 39,
huku moja likitiwa kambani na `Diego wa Kampala`, Khamis Friday Kiiza
anayecheza Yanga ya Dar es salaam kwa mkwaju wa penati dakika ya 19 ya
mchezo.
Ushindi
huo unaifanya Uganda ifikishe pointi 6 kutokana na matokeo ya awali ya
ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Amavubi na kupanda kileleni mwa kundi hilo
kwa wastani mzuri wa mabao ya kufunga na kufungwa, kwani hata Sudan
wanazo alama 6 kibindoni.
Mchezo wa mapema uliwakutanisha Rwanada na Sudan na kushuhudia Amavubi wakila `nakozi` ya bao 1-0 tena kutoka kwa Sudan.
Matokeo
hayo ni mabaya zaidi kwa Rwanda huku Nahodha wake, Haruna Niyonzima
akishikwa na machungu zaid kutokana na mchezaji mwenzake wa Yanga,
Khamis Kiiza kuendelea kudunda kwa raha zake.
Bao hilo pekee na muhimu zaidi kwa Sudan limefungwa katika dakika ya 29 kupitia kwa Salah Ibrahim.
Matokeo
ya leo yanaiweka Rwanda katika mazingira magumu ya kusonga mbele hatua
ya robo fainali kwani mchezo wa awali walikalia cha mtema kuni baada ya
kulambishwa bao 1-0 na Uganda.
Katika
kundi A, wenyeji Harambee Stars na wahabeshi wa Ethiopia wapo nafasi
nzuri ya kwenda robo fainali na Zanzibar heroes inayoshika nafasi ya
tatu, inaweza kuangukia katika kuwania moja ya nafasi mbili za best
losers.
Iwapo Zanzibar itaifumua Harambee Stars watawania Robo Fainali katika nafasi mbili za best loosers.
Kundi B Zambia imejihakikishia kwenda Robo Fainali na mechi baina ya Tanzania Bara na Burundi itaamua timu ya kuungana na mabingwa hao wa zamani wa Afrika na ya kuwania kufuzu kwa nafasi za best losers.
Kundi B Zambia imejihakikishia kwenda Robo Fainali na mechi baina ya Tanzania Bara na Burundi itaamua timu ya kuungana na mabingwa hao wa zamani wa Afrika na ya kuwania kufuzu kwa nafasi za best losers.
Michuano hiyo itaendelea kesho kwa timu za kundi A kushuka dimbani kuwania mzigo wa pointi tatu muhimu.
Mechi
ya mapema itawakutanisha Sudan Kusini dhidi ya Ethiopia, wakati wenyeji
wa michuano ya mwaka huu, timu ya Taifa ya Kenya, Harambee Stars
itamenyana na mashujaa wa visiwani, Zanzibar Heroes.
No comments:
Post a Comment