Na Frank Mvungi
Taasisi yaTiba ya Mifupa na Mishipa ya Fahamu (MOI) imepanga kutumia zaidi ya Bilioni 17 katika ujenzi wa awamu ya Tatu ya Mradi wa Taasisi yaTiba ya Mifupa na Mishipa ya Fahamu (MOI phase 111) hadi mradi huo utakapokamilika mapema mwakani.
Hayo
yamesemwa leo na Meneja Uhusiano wa Taasisi hiyo Bw. Jumaa Almasi
wakati akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam.
Almasi
alisema kuwa Ujenzi wa jengo hilo jipya lenye ghorofa 7 ambao
unaendelea ukikamilika utaongeza maeneo ya kutolea huduma,Vitanda
vitafikia 380 kutoka 159 vilivyopo sasa hali ambayo itapanua wigo wa
huduma zinazotolewa kwa sasa.
“Mradi
huu utasaidia kuongeza ufanisi na huduma zinazotolewa na taasisi kwani
ukikamilika utaongeza maeneo ya kutolea huduma kwa kupunguza msongamano
wa wagonjwa mawodini kutokana na kuongezeka kwa vitanda kutoka 159 hadi kufikia 380” Alisema Almasi.
Aliongeza
kuwa huduma nyingine zitakazotolewa ni CT SCAN,MRI,huduma za Cybernife
na Digital Antiograph ambazo kwa Sasa hazitolewi katika Taasi hiyo .
Alibainisha
kuwa MOI ni moja ya Taasisi zenye vifaa bora vya upasuaji pamoja na
vyumba vya upasuaji vinavyokikidhi viwango vya kimataifa kusini mwa
jangwa la Sahara baada ya Afrika ya kusini.
Alisema
kuwa hali hiyo ni matokeo ya juhudi kubwa zinazofanywa na Serikali
katika kuboresha huduma za afya nchini ambapo wameweza kupatiwa vifaa
vya kisasa pamoja na wataalamu waliobobea katika huduma za tiba ya
mishipa ya fahamu na upasuaji wa uti wa mgongo.
Bw.
Almasi alibainisha kuwaTaasisi ya MOI imeendelea kushirikiana na
Taasisi za Kimataifa zinazotoa huduma za afya kama SIGN GROUP ya
nchini Marekani ambayo imekuwa ikitoa msaada wa vifaa tiba ikiwa ni
alama ya ushirikano mzuri uliopo kati ya Taasisi hiyo na mashirika ya
Kimataifa.
No comments:
Post a Comment