Naibu
Katibu Mkuu wa UWT Zanzibar Bi. Salama Abuud Talib akimkaribisha Makamu
Mwenyekiti UWT Bi. Asha Bakari Makame kuzungumza na wandishi wa Habari
kuhusu miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa upande wa Jumuiya hiyo.
Makamu
Mwenyekiti UWT Bi. Asha Bakari Makame akizunguza na wandishi wa Habari
kuhusu miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui
Mjini Zanzibar.
Makamu
Mwenyekiti UWT Bi. Asha Bakari Makame akisisitiza kitu alipokuwa
akizungumza na wandishi wa Habari kuhusu miaka 50 ya Mapinduzi ya
Zanzibar ofisini Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini
Zanzibar.
Zanzibar.
Mwandishi
wa Habari wa Chuchu Fm Radio Rahama Suleiman akitaka ufafanuzi wa kitu
kwenye Mkutano wa UWT ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Zanzibar.
(Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar).
Na Ali Issa Maelezo-Zanzibar
Umoja
wa wanawake wa CCM Tanzania (UWT) umesema vikundi vingi vya ushirika
vya kina mama vimesaidiwa fedha nyingi za mikopo kujiendesha lakini
inaonekana bado kuna baadhi ya kinamama wanashindwa kuviendesha vikundi
hivyo kutokana na kutokuwa na dira nzuri kuviendeleza vikundi hivyo.
Hayo
yamesemwa leo huko ofisi kuu ya Chama cha Mapinduzi Kisiwandui Mjini
Zanzibar na Naibu Katibu Mkuu wa UWT Zanzibar Salama Aboud Talib wakati
alipokuwa na mazungumzo na waandishi wa Habari katika kuadhimisha
sherehe za miaka 50 ya mapinduzi Zanzibar kwa Jumuiya ya wanawake wa CCM
Zanzibar.
Amesema
umoja wa wanawake Tanzania kupitia wake wa viongozi wa kuu wa Serikali
na tasisi nyengine wametoa pesa nyingi katika kusaidia vikundi vya
kinamama ili kujikwamua na umasini na kuviendeleza vikundi vyao kupata
tija jambo ambalo baadhi ya viongozi wa vikundi hivyo hushindwa
kuviendeleza na hatimae kutofikia malengo ya kuazishwa kwake.
Amesema
hali hiyo si njema kwani inarudisha nyuma juhudi za viongozi jambo
ambalo lengo la chama cha Mapinduzi ni kuijenga jamii ya wanawake kua na
muelekeo mzuri kimaendeleo na kujinasua na umasikini.
“Wake
waviongozi wetu huwapa pesa nyingi wana vikundi kuwasaidia wanawake
lakini vikundi hivyo hushindwa kuziendeleza pesa zile na baadae
kikundi huwa kina shindwa kujiendeshana pesa kupotea,” alisema Salama.
Aidha
alifahamisha kuwa wanashindwa kufahamu kupotea kwa pesa hizo kwani
amesema kabla ya kutolewa peasa hizo vikundi hupatiwa mafunzo kutoka kwa
wataalamu ili waweze kuviendesha.
Bi.Salama
alisema hali hiyo haifurahishi hata kidogo kuona pesa zinapotea na
vikundi kufa na italazimika kwa wanavikundi kutafuta mbinu mbadala
badala ya zile za kitalamu ili kuona vikundi vina piga hatukubwa za
kimaendeleo.
Nae
Makamo mwenyekiti UWT Bi. Asha Bakari Makame alisikitishwa sana na
suala la unyanyasaji kwa watoto na wanawake na kuishauri Serikali
iangalie kwa umakini suala hilo kwani inaonekana kuna mtandao mkubwa wa
kuwadhalilisha watoto kwa kuwanajisi hali ambayo ni hatari katika taifa
hili la Zanzibar.
Amesema
Serikali iangalie sheria zake na kuzifanyia marekebisho kwani watoto
wanaharibiwa vibaya na watuhumiwa kushindwa kuingia hatiani jambo ambalo
sisahihi kwa watoto kudhalilishwa kwa kunajiwa na kutengwa na
wazaziwao.
Makamo
huyo alisifu juhudi za Jumuiya hiyo inazochukua kwa kua karibu na wana
nchi kupitia Serikali kuu kwa kufuata ilani ya chama cha Mapinduzi.
Alisema
hivi sasa wanawake wa Zanzibar wamefaidika sana na Jumuiya hiyo kwa
kupata frusa katika ngazi za Sekikali na kuweza pia kupata elimu na
ajira kwa idadi ya wanawake ambayo ni wazi kuwa wanwake wa Zanibar
wanathaminiwa sana na serikali yao.
Bi.Asha
Bakari alizipongeza Serikali zilizo pita,Viongozi wa Afroshirazi na hii
ilioko madarakani kwa kuyaendeleza Mapinduzi matukufu yalio mkomboa
mwanamke kutoka katika utwala wakisultani na 1964 kua Taifa huru,lenye
Umoja amani na mshikamano.
No comments:
Post a Comment