Wakandarasi na Washauri wakiwa wanamsikiliza kwa makini Mtendaji Mkuu wa TANROADS mhandisi Patrick Mfugale (hayupo pichani). Mameneja wa TANROADS toka Mikoa mbalimbali ya Tanzania wakiwa wamehudhuria sherehe za kuweka saini mikataba hiyo.
Baadhi
ya wabunge wanaotoka katika mikoa ambayo miradi hiyo ya ujenzi wa
barabara itafanyika wakishuhudia sherehe za kutia saini mikataba ya
ujenzi wa barabara hizo mapema hii leo jijini Dar
Mwakilishi
toka Benki ya Maendeleo ya Afrika bwana Patrick Musa akielezea mipango
ya Benki hiyo kuendelea kutoa mikopo katika maradi mbalimbali ya
maendeleo nchini.
Mwakilishi
wa Shirika la Maendeleo la Japan (JICA) Bwana Onishi Yasunori akieleza
mikakati ya shirika hilo kutoa mikopo katika shughuli mbalimbali za
maendeleo hapa nchini huku akionesha moja ya ramani ya ujenzi
wanaotarajia kufanya hapa nchini.
Waziri
wa Ujenzi Dkt John Magufuli akisistiza jambo kwa waandishi wa
wakandarasi mapema hii leo jijini Dar es Salaam, wakati wa utiaji saini
mikataba mitatu ya ujenzi wa barabara.
Mtendaji
Mkuu wa TANROADS Mhandisi Patrick Mfugale (wa pili kulia) akiweka saini
Mkataba ujenzi wa barabara ya Mayamaya hadi Mela, wa pili kulia ni
mwakilishi wa Kampuni ya china Henan International Cooperation Group Co.
Ltd. Bwana Ghuo Zhijian, kulia ni Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo
la Japan (JICA) Bwana Onishi Yasunori na kushoto ni Mwakilishi toka
Benki ya Maendeleo ya Afrika bwana Patrick Musa.
Picha Zote na Eliphace Marwa – MAELEZO
Na Eliphace Marwa (Maelezo)
Serikali
imetia saini mikataba mitatu ya ujenzi wa barabara yenye thamani ya
zaidi ya shilingi bilioni Tsh.538 za Kitanzania kwa ushirikiano toka
Benki ya Maendeleo ya Afrika (ADB) na Shirika la Maendeleo la Japan
(JICA) mapema hii
Akizungumza
leo jijini Dar es Salaam wakati wa sherehe za kutia saini mikataba
hiyo,Mtendaji Mkuu wa TANROADS Mhandisi Patrck Mfugale alisema kati ya
fedha hizo ADB wanachagia asilimia 65.80 , JICA asilimia 29.2 ambazo
wametoa mkopo na Serikali inachangia asilimia tano.
“Mikataba
iliyotiliwa saini hii leo ni pamoja na ujenzi wa sehemu ya Mayamaya
hadi Mela yenye urefu wa kilomita 99.35 inayojengwa na Kampuni ya China
Henan International Cooperation Group Co. Ltd (CHICO) kwa gharama ya
zaidi bilioni mia moja kwa muda wa miezi thelasini na sita,” alisema
Mfugale.
Alizitaja
barabara nyingine ni Mela hadi Bonga yenye urefu wa kilomita 88.8
inayojengwa na Kampuni ya China Railway Seventh Group kwa gharama ya
zaidi Sh. bilioni 88 , ambapo muda wa utekelezaji ni miezi thelasini na
sita.
Mkataba
wa mwisho ni wa ujenzi wa barabara ya Mangaka hadi Mtambaswala yenye
urefu wa kilomita 65.5 itakayojengwa na Kampuni ya Sichuan Road and
Bridge (Group) Corporation kwa gharama ya zaidi ya Sh.bilioni 59 na muda
wa utekelezaji ni miezi ishirini na nne.
“Napenda
kuwapongeza Benki ya Maendeleo ya Afrika pamoja na Shirika la Maendeleo
la Japan kwa ushirikiano wao kwani sio mara ya kwanza kutupatia mkopo
kwa ajili ya ujenzi wa barabara zetu na tunaahidi kuzisimamia ili ziwe
katika ubora unaotakiwa”, alisema Mfugale.
Aidha
naye Waziri mwenye dhamana ya ujenzi Dkt. John Magufuli alishukuru ADB
na JICA kwa mkopo huo na kutoa angalizo kwa wakandarasi wasio makini na
kazi zao kukaa chonjo kwani sasa hakuna huruma kwao tena.
“Napenda
kuwatahadharisha nyie makandarasi mlioko hapa kama kuna yeyote kati
yenu hataweza kufanya kazi kwa ubora na wakati basi asisaini mkataba
huu”, alisema Dkt Magufuli.
Nao
wawakilishi toka ADB na JICA walimshukuru Waziri Magufuli kwa
usimamizi imara wa miradi mbalimbali ujenzi inayoendelea kote nchini.
Hii
si mara ya kwanza kwa ADB na JICA kutoa mkopo kwa ajili ya ujenzi wa
barabara kwani Machi mwaka , 2010 walitoa mkopo kwa ajili ya ujenzi
wa barabara za Iringa mpaka Dodoma yenye urefu wa kilomita 260 na
barabara ya Namtumbo mpaka Tunduru yenye urefu wa kilomita 193.
No comments:
Post a Comment