Marehemu Nelson Rolihlahla Mandela enzi za uhai wake.
Rais
wa zamani wa Afrika Kusini, Nelson Mandela amefariki dunia muda mfupi
uliopita akiwa na umri wa miaka 95 jijini Johannesburg, Afrika Kusini.
Rais wa nchi hiyo, Jacob Zuma amethibitisha taarifa hizo!
Rais Zuma amesema "taifa limepoteza mtu muhimu" na kuongeza "kwa sasa amepumzika. Yupo mahala pema"
Mzee Mandela aliyekuwa akisumbuliwa na homa ya mapafu amefariki akiwa amezungukwa na familia yake nyumbani kwake Johannesburg.
Mandela atazikwa kitaifa na bendera zitapepea nusu mlingoti alisema Rais Zuma.
Alikuwa
akipatiwa matibabu kwa takribani miaka mitatu iliyopita na hali yake
ilibadilika zaidi katika miezi sita ya mwisho kabla ya kifo chake.
Mpiganaji
huyo wa ubaguzi wa rangi, aliingia Ikulu ya Afrika Kusini akiwa mtu
mweusi wa kwanza kuiongoza nchi hiyo mwaka 1994 mpaka 1999 baada ya
kutumikia kifungo cha miaka 27 gerezani.
Rais wa Jamhuri Ya Muungano wa
Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemtumia Salamu za
rambirambi Rais Jacob Zuma wa Afrika ya Kusini na kupitia kwake, kwa
mkewe Bi. Graca Machel, wanafamilia wote na wananchi wote wa Afrika ya
Kusini kufuatia kifo cha Mzee Nelson Mandela kilichotokea tarehe 5
Desemba, 2013 baada ya kuugua kwa muda mrefu.
Rais ameuelezea msiba huu kuwa ni msiba mkubwa kwetu sote.
"Afrika ya Kusini, Afrika na dunia kwa ujumla imepoteza mtu mashuhuri na shujaa mkubwa wa Karne ya 20 na 21.Tunaelewa machungu waliyonayo wananchi wa Afrika ya Kusini kwa kupoteza kiongozi shupavu, jasiri, mwana mapinduzi , mvumilivu na mstahimilivu". Ameongeza Rais Kikwete.
Rais ameuelezea msiba huu kuwa ni msiba mkubwa kwetu sote.
"Afrika ya Kusini, Afrika na dunia kwa ujumla imepoteza mtu mashuhuri na shujaa mkubwa wa Karne ya 20 na 21.Tunaelewa machungu waliyonayo wananchi wa Afrika ya Kusini kwa kupoteza kiongozi shupavu, jasiri, mwana mapinduzi , mvumilivu na mstahimilivu". Ameongeza Rais Kikwete.
Kufuatia kifo hicho Rais ametangaza siku 3 za maombolezo kuanzia leo tarehe 6 hadi 8 Disemba, 2013. Aidha, Mheshimiwa Rais ameagiza kuwa katika siku hizo 3 bendera zote zipepee nusu mlingoti.
Wengine
waliotuma salam za rambi rambi ni pamoja na rais Barack Obama wa
marekani na Waziri Mkuu wa Uingereza, David Cameron amesema: "taa kubwa
imezimika duniani
"Nelson Mandela alikuwa shujaa"
"Nelson Mandela alikuwa shujaa"
No comments:
Post a Comment