Rais Jakaya Kikwete, ameaonya wanasiasa nchini kuingiza mambo ya siasa kwenye kilimo, hasa kilimo cha mkataba kwa wakulima.
Alitoa onyo juzi mjini Nyashimo, wilayani Busega, katika siku yake ya mwisho ya ziara ya siku tano katika Mkoa mpya wa Simiyu.
Rais
Kikwete alisema kuna baadhi ya wanasiasa, wamekuwa wakiyatumia majukwaa
kupotosha ukweli juu ya manufaa ya kilimo cha mkutaba kwa mkulima,
badala ya kuwaelimisha, nini manufaa ya kilimo hicho.
Akiwahutubia
mamia ya wakazi wa mji mdogo wa Nyashimo, Rais Kikwete alisema
wanasiasa hao hawana tofauti na wakoloni, ambao mikataba yao ilikuwa ni
za kumkomoa mzalendo, kwa mikataba isiyo na tija kwa mwananchi.
Alionya
kuwa kamwe wanasiasa wasipambane na kilimo hicho, kwa sababu ya manufaa
yao binafsi ya kisiasa na badala yake waangalie ni kwa namna gani
atanufaika na kilimo cha mkataba.
Badala
yake, Rais Kikwete aliwataka wanasiasa na viongozi wote kutoa elimu kwa
wakulima juu ya manufaa ya kilimo cha mkataba kinacholenga kuwakomboa.
Akizungumzia
ruzuku ya mbegu ya pamba, Rais alionyesha kusikitishwa kwake ni jinsi
gani ruzuku hiyo imeoendolewa, na kuahidi kutafuta mwarobaini wa kilio
cha wakulima wa zao la pamba wakiwamo wa mkoa wa Simiyu.
“Ile
ruzuku ya mbegu ya pamba mbona imeondoka, nitawauliza wahusika…niachieni
mimi na majibu yake mtayapata msimu unaofuta,” alisema.
Kuhusu
mbegu za pamba ya manyonya na isiyo na manyoya, Rais Kikwete alisema
wataalam na viongozi katika maeneo yao, hawanabudi kuwaeilimisha
wakulima manufaa ya kupanda mbegu bora yenye uzalishaji wenye tija.
Kuhusu
wafugaji, aliwataka wanasiasa kuacha kushabikia ufugaji wa kuhamahama
na kueleza kuwa kamwe serikali haitawavumilia hasa wenye tabia ya
kuvamia maeneo ya wakulima na kusababisha uharibifu wa mazingira.
CHANZO: NIPASHE
No comments:
Post a Comment