Na Baraka Mpenja - Dar es salaam
Wakati
timu ya Taifa ya vijana ya wanawake chini ya miaka 20, maarufu kwa jina
la Tanzanite ikijiandaa na Mechi ya kwanza ya raundi ya michuano ya
Kombe la Dunia, Kanda ya Afrika dhidi ya Afrika Kusini Uwanja wa Taifa,
Dar es Salaam Desemba 7 mwaka huu, kocha mkuu wa timu za taifa za
wanawake , Tanzanite na Twiga stars, Rogasian Kaijage amewaomba
watanzania kuwatia moyo vijana hawa kwani hawajaanza kufanikiwa bado.
Kaijage
amesema watanzania wasitegemee mafanikio ya haraka kwa timu hii na wale
wasichukulie matokeo ya mwanzo kama mafanikio, bali wanatakiwa kuwapa
moyo vijana hawa kwani safari yao ni ndefu mno.
“Watanzania
tusiwae na tabia ya kutaka mafanikio ya haraka, hawa vijana bado wanayo
safari ndefu, cha msingi watanzania hasa wapenda michezo wawape sapoti
kubwa ili kufikia mafanikio”. Alisema Kaijage.
“Vijana
hawa ni mahindi machanga ndio yanaanza kuchipua, kile wanachokifanya
sio mavuno bali ni ishara kuwa wanatakiwa kuungwa mkono. Hawatakiwi
kukatishwa tamaa, waungwe mkono kwani wanatengenezwa kwa ajili ya
baadaye”. Aliongeza Kaijage.
Kocha
huyo alisema katika soka lazima mipango iwekwe, watu wakubali kuwekeza,
hivyo wapende michezo wajitokeza kudhamini timu za wanawake kwani wanao
uwezo wa kufika mbali zaidi.
Akizungumzia
mchezo ujao dhidi ya Afrika kusini, Kaijage alisema utakuwa mgumu sana
kutokana na ubora wao, lakini kila kitu kinawezekana kutokana na
maandalizi ya vijana wake.
“Vijana
wanaendelea vizuri sana, ninaposema hivyo namaanisha wana morali ya
kushindani ili kupata matokeo mazuri. Hivyo watanzania wajiandae kuwapa
sapoti vijana wao”. Alisema Kaijage.
Tanzanite
ilifuzu raundi ya pili baada ya kuifunga Msumbiji mabao 15-1 ambapo
mechi ya kwanza jijini Dar es salaam waliwalamba 10-0 na mechi ya
msumbiji wakaitungua 5-1.
No comments:
Post a Comment