Dar
es Salaam: Mechi ya Nani Mtani Jembe kati ya Simba na Yanga
zinazodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager itachezwa Jumamosi, Desemba
21, 2013 saa kumi kamili jioni kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es
salaam.
Akiongea
na waandishi wa habari jijini Dar es salaam leo, Meneja wa Kilimanjaro
Premium Lager, George Kavishe amesema “Tayari Simba na Yanga zimesaini
makubaliano ya kucheza MECHI YA NANI MTANI JEMBE (NANI MTANI JEMBE
MATCH). Pambano hili ni zawadi ya kufungia mwaka kwa mashabiki na kila
timu imetia sahihi makubaliano kwamba itachezesha kikosi cha kwanza ili
kuwapa mashabiki burudani ya uhakika.”
Kavishe
aliongeza kuwa mechi hii ni maalum kwa ajili ya kuhitimisha kampeni ya
Nani Mtani Jembe ambayo imeendeshwa kwa zaidi ya miezi miwili ikiwapa
fursa mashabiki wa timu hizi kuchangia timu zao kila wanapoburudika na
bia ya Kilimanjaro Premium Lager.
Kilimanjaro
Premium Lager ilitenga kiasi cha shilingi milioni 100
zinazoshindaniwa na Simba na Yanga kupitia mashabiki wake na tarehe 21
Desemba ndio utakuwa mwisho wa kampeni ya Nani Mtani Jembe ambapo baada
ya mechi fedha hizo zitagawanywa kwa kila timu kulingana na matokeo ya
kura za mashabiki na klabu zitajiamulia namna ya kutumia fedha hizo.
Kampeni
hii imeleta msisimko mkubwa sana kati ya mashabiki na hadi sasa matokeo
ya kampeni hii yanaonyesha kwamba Yanga wanaongoza wakiwa na kiasi cha
shilingi milioni 76 huku Simba wakiwa na kiasi cha shilingi milioni 24
Mashabiki
wa Simba na Yanga wanaoshiriki katika kampeni ya Nani Mtani Jembe
wanaendelea kunufaika zaidi na zawadi kabambe zilizoandaliwa na bia ya
Kilimanjaro Premium Lager ili kuongeza msisimko na ushiriki katika
kampeni hiyo ambapo mashabiki watatu wa Simba na mashabiki watatu wa
Yanga wanajishindia kiasi cha shilingi 300,000/= kila mmoja katika droo
zinazofanyika mara moja kila wiki. Droo kubwa itafanyika tarehe 21
Desemba. Ambapo katika droo hiyo kubwa shilingi milioni 6 zitatolewa
kama zawadi kwa washindi wawili – mmoja shabiki wa Yanga na mwingine
shabiki wa Simba ambapo kila mmoja atajishindia shilingi milioni tatu.
No comments:
Post a Comment