Na Kiza Sungura- MAELEZO_Dar es salaam
Shirika
la Madini la Taifa [STAMICO] limeingia mkataba wa ubia na Kampuni ya
TanzaniteOne Mining Limited [Tanzanite One] kuhusu uchimbaji wa pamoja
wa madini, ya Tanzanite katika kitalu C, Mirerani.
Kauli
hiyo ilitolewa jana mjini Dar es salaam na Mkurugenzi Mkuu wa STAMICO
Gray Mwakalukwa wakati akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari mara
baada ya hafla fupi ya kusaini mkataba huo.
Mwakalukwa
alisema kuwa hatua hiyo imefikiwa baada ya Serikali kupitia Wizara ya
Nishati na Madini kutoa leseni ambayo inawawezesha STAMICO kumiliki
asilimia 50 na TanzaniaOne watabaki na asilimia 50.
Alisema
kuwa umiliki huo unatokana na Serikali kusimamia utekelezaji wa Sera ya
Madini ya mwaka 2009 na Sheria ya Madini ya mwaka 2010 ambapo chini ya
sharia hiyo, Kampuni za kigeni haziruhusiwi kumiliki hisa zaidi ya
asilimia 50 katika uchimbaaji wa vito.
Mwakalukwa
aliongeza kuwa mkataba huo umezingatia makubaliano ya awali yaliyotiwa
saini mapema mwaka huu ambayo yataka STAMICO na Tanzanite One kuwa na
gawio sawa la asilimia 50 kwa hamsini litakalotokana na faida.
Alitaja
baadhi ya mambo waliokubaliana ni pamoja na mitambo ya uchimbaji na
uzalishaji itabaki kuwa ni mali ya Tanzanite One itaendelea kutumika na
wabia wataifanyia matengenezo itakapoharibika.
Mwakalukwa
alisema kuwa jambo jingine waliokubaliana ni pamoja na kuanzisha
kitengo maalum cha ufuatiliaji na tathmini ya shughuli zote za mgodi
kitakachoundwa kutoka kwa wajumbe wa kila pande.
Naye
Mwenyekiti wa Tanzanite One, Balozi Ami Mpungwe alisema kuwa hatua ya
Kampuni yake kusaini mkataba huo ni sehemu ya kutekeleza sera ya
uchimbaji wa madini nchini na ni hatua nzuri ya kuhakikisha ulinzi
na usalama madini ya Tanzanite.
No comments:
Post a Comment