Kibaha.
Mwenyekiti wa mfuko wa fursa sawa kwa wote, Mama Anna Mkapa ametoa wito
kwa jamii kushiriki kuwasaidia watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu
ili kupata mahitaji yao muhimu kama walivyo wengine.
Mama
Mkapa alitoa wito huo jana Mjini Kibaha wakati akipokea msaada wa vitu
mbalimbali vyenye thamani ya Sh7 milioni vilivyotolewa na Umoja wa
Wafanyabiashara wa China kwenye kijiji cha kulelea watoto yatima Kibaha.
Akizungumza
wakati akipokea msaada huo, alisema kuna haja ya kila mtu kusaidia
watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu ili waweze kuishi kwenye vizuri
kama walivyo watoto wenye wazazi.
“Naomba
kila mtu na kila jamii itambue umuhimu wa kuwasaidia watoto wanaoishi
kwenye mazingira magumu, kwani watoto hawa ni wetu sote,” alisema Mama
Mkapa.
Mama Mkapa alishukuru umoja huo kwa kutoa msaada huo ambao utasaidia kuongeza nguvu kwenye kituo hicho.
Naye
mwakilishi wa Umoja huo wa wafanyabiashara hao Wachina, Hu- Jianxi
alisema kuwa wameguswa kuwasaidia watoto hao kwani wanahitaji kusaidiwa
ili nao wajisikie kama jamii za watoto wengine wanaolelewa na wazazi
wao.
No comments:
Post a Comment