Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akikata utepe kuzindua mradi wa nyumba za
watumishi wa afya zilizojengwa na Taasisi ya Mkapa Foundation katika
hafla iiyofanyika katika kijiji cha Matemanga wilayani Tunduru Mkoani
Ruvuma leo.
Jumla
ya nyumba 480 zinajengwa katika halmashauri 48 nchini na miongoni mwa
nyumba hizo 40 zipo katika mkoa wa Ruvuma.Taasisi ya Benjamin Mkapa
iliingia mkataba na Wizara ya Afya kutekeleza mradi wa miaka
mitano(2011-2016) wa uimarishaji wa mifumo ya Huduma za afya chini ya
ufadhili wa mfuko wa Dunia wa kupambana na ukimwi,kifua kikuu na
Malaria(Global Fund).
Wengine
katika picha kutoka kushoto ni Mke wa Rais Mama Salma Kikwete, Afisa
Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Benjamin W.Mkapa Dkt.Ellen Senkoro, Mbunge
wa Jimbo la Tunduru Mhandisi Ramo Makani, Meneja wa Portfolio, Mfuko wa
Dunia wa Kupambana na ukimwi,kifua kikuu na Malaria Bi. Tatajana
Peterson, Waziri wa Ardhi Nyumba na Makazi Prof.Anna Tibaijuka, Naibu
Waziri wa TAMISEMI Aggrey Mwanri, Naibu waziri wa Afya na Ustawi wa
jamii Kebwe Stephen Kebwe, na kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Bwana
Saidi Mwambungu.
Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kiwete akiteta jambo na mkazi wa kijiji cha Ligela
wilayani Namtumbo Bwana Edwin Ngonyani wakati alipokuwa anahitimisha
ziara yake wilayani humo.Bwana Ngonyani ambaye alipata ulemavu baada ya
kupoteza miguu yote miwili katika ajali ya moto alimweleza Rais kuwa
anapata taabu ya kutafuta riziki kwakuwa anatambaa kwa taabu.Rais
Kikwete alitoa ahadi ya kumsaidia mlemavu huyo ili aweze kujikimu
kimaisha.
Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia wananchi wa kijiji cha Matemanga
wakati wa hafla ya uzinduzi nyumba 480 za watumishi wa umma zilizojengwa
na Taaasisi ya Benjamin W.Mkapa kwa ushirikiano na Wizara ya Afya
Afisa
Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Benjamin w.Mkapa Dkt Ellen Mkondya
Senkoro(kushoto) akimuonesha Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete michoro na
ramani za nyumba za watumishi wa afya zilizojengwa na taasisi hiyo wkati
hafla ya uzinduzi wa nyumba hizo uliofanyika katika kijiji cha
Matemanga wilayani Tunduru leo.Watatu kushoto ni Naibu Waziri wa Afya
Dkt. Kebwe Stephen Kebwe na wane kushoto ni Waziri wa Ardhi Nyumba na
Makazi Profesa Anna Tibaijuka.Picha na Freddy Maro
No comments:
Post a Comment