Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais - Mazingira Dkt.
Injinia Binilith Satano Mahenge (wa pili kulia), akipata maelezo kutoka kwa
Mkurugenzi wa uzalishaji soda Bw. Louis Coetzee ( wa kwanza kulia), akielezea jinsi
kiwanda hicho kinavyotumia maji taka kulinda Mazingira ya kiwanda.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais- Mazingira Dkt.
Injinia Binilith Mahenge, akiongea na Vyombo vya habari kuhusu ziara yake na
kuwaambia kwamba nchi inahitaji wawekezaji wanaotunza na kulinda Mazingira
yetu. Viwanda alivyovitembelea ni kiwanda cha kuzalisha Mafuta ya kula na
sabuni (BIDCO), M.M.I steel mill kinachozalisha Nondo na Mabati pamoja na
kiwanda cha Coca Cola vilivyopo Mikocheni
jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais - Mazingira Dkt.
Injinia Binilith Satano Mahenge, akizungumza na Menejimenti ya kiwanda cha Coca
Cola (hawapo pichani) kuhusu kiwanda
hicho jinsi walivyoweza kutunza Mazingira na kuwataka waendelee kuboresha zaidi
Mazingira ya kiwanda na kuwa mfano wa kuigwa kwa viwanda vingine.
Maji machafu yenye kemikali
yanayotiririka kutoka kwenye kiwanda kinachozalisha Nondo na Mabati (M.M.
I steel mill ) kilichopo mikocheni jijini Dar es Salaam ambayo si salama kwa
wananchi na mazingira kwa ujumla.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais - Mazingira Mh. Dkt.
Injinia Binilith Satano Mahenge ( wa pili
kulia) pamoja na Mkurugenzi wa Mazingira
Ofisi ya Makamu wa Rais Bw. Julius Ningu (wa kwanza kushoto), wakiwa katika
ziara fupi ya ukaguzi wa mazingira
katika kiwanda cha Coca Cola kilichopo Mikocheni jijini Dar es Salaam. Wakiwa
pamoja na mkurugenzi wa uzalishaji soda katika kiwanda hicho Bw. Louis Coetzee (wa
kwanza kulia).
========== ======= ========
Wawekezaji
wote Nchini wanatakiwa kuhakikisha wanaacha kutumia magogo katika
uzalishaji badala yake watumie tekinolojia ya kisasa ili kuepuka
mabadiliko ya tabia ya nchi na uchafuzi wa Mazingira yanayotokana na
ukataji miti.
Hayo yamesemwa jijini Dar
es Salaam na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mh.Dkt. Injinia
Binilith Mahenge wakati alipofanya ziara ya kutembelea kiwanda cha
kutengeneza sabuni na mafuta ya kupikia (BIDCO) kilichopo mikocheni
jijini Dar es Salaam.
Amekiagiza kiwanda
hicho kuacha mara moja matumizi ya magogo kwani inaathari kubwa sana kwa
jamii. Hata hivyo amesema kuwa atatembelea tena kuangalia kama
wameacha kutumia magogo ndani ya miezi sita, endapo watabainika
wanaendelea kutumia magogo,hatua kali itachukuliwa juu ya Kiwanda hicho
endapo watakiuka masharti waliyopewa Kiwanda kitafungwa mara moja.
Hata hivyo Mh. Mahenge
amewaomba wawekezaji wa viwanda vingine kuiga mfano wa kiwanda cha Coca
Cola katika utunzaji wa Mazingira, kwani wao ni mfano mzuri kwa viwanda
vingine kwa kuanzisha technolojia nyengine ya kuchunguza maji taka kama
ni salama kwa viumbe hai.
No comments:
Post a Comment