Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu mchimati@gmail.com au namba +255767869133.
Mfuko wa Pensheni kwa Umma (PSPF)
Akikabidhi msaada huo jana, Mwakilishi wa mfuko huo Mkoa wa Ruvuma,
Deogratius Njuu, alisema, PSPF ni mdau mkubwa wa elimu wamegushwa na
tatizo hilo hivyo wameona wasaidiane na halmashauri hiyo ili kupunguza
tatizo hilo.
Njuu ameongeza kuwa, mfuko huo unaamini kuwa taifa lolote lenye
maendeleo lazima libebwe na elimu na ndiyo maana nao wamepanga kusaidia
katika kuinua kiwango cha elimu katika maendeleo mbali mbali nchini.
Aidha, amewashauri kuyatunza madawati hayo ili yaweze kudumu kwa muda mrefu na kuwasaidia wanafunzi wote.
Kwa upande wake Mbunge wa jimbo la Tunduru Kaskazini, Ramo Makani,
amewapongeza PSPF kwa kutoa msaada huo kwa kuwa utasaidia kupunguza
tatizo la madawati na kuwataka wadau wengine watakao sikia waige mfano
mzuri na bora uliofanywa na mfuko huo.
Alisema, bado halmashauri inakabiliwa na changamoto nyingi kama
upungufu wa madawati ambapo watoto wa shule za msingi wanakaa chini,
upungufu wa matundu ya vyoo, meza, viti pamoja na miundombinu, hivyo
amewaomba watu wenye uwezo wasaidiane na halmashauri kutatua matatizo
hayo.
Naye Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru, Kenneth
Haule, alisema kuwa halmashauri hiyo ina upungufu wa madawati 4537 ili
kufanikisha utoaji elimu bora kwa watoto ni muhimu kuwapo kwa
miundombinu na samani za kutosha zenye viwango kwa wanafunzi na walimu.
Alisema, wilaya hiyo inaupungufu mkubwa wa miundombinu na samani za
kielimu vyumba vya madarasa, nyumba za walimu, vyoo pamoja na madawati
ambapo jitihada kubwa za kupunguza tatizo hilo kwa kushirikiana na
serikali kuu na jamii husika bado zinaendelea kutokana na ongezeko
kubwa la wanafunzi wanaosajiliwa kila mwaka.
Aidha, alisema bado wilaya ina upungufu mkubwa wa samani za shule
hivyo ameomba waendelee kusaidia kila wanapopata fursa ili kuendeleza
sekta ya elimu nchini.
CHANZO:
NIPASHE
No comments:
Post a Comment