Mbunge wa Iringa Mjini
Mchungaji Peter Msigwa akikabidhi msaada wa Sukari, kwa Kaimu Shekhe
Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Abubakari Chalamila kwa ajili ya kituo cha
Kitanzani Islamic center kilichoko mjini Iringa.
Baadhi ya misaada iliyotoa mbunge wa Iringa mjini mch. Peter Msigwa kwa kituo cha chuo cha Kitanzani Islamic center kilichoko
mjini Iringa. (Picha zote na Denis
Mlowe).
Na Denis Mlowe,Iringa
MBUNGE wa Iringa
Mjini(Chadema) Mchungaji Peter Msigwa amekikabidhi chuo cha Kitanzani Islamic
Center msaada wa Sukari,Unga wa Ngano, tende na mafuta ya kupikia ikiwa ni
utaratibu wake wa kila mwaka kukisaidia chuo hicho.
Akizungumza wakati wa
kukabidhi msaada huo jana kwa Shekhe Mkuu wa Mkoa Iringa Abubakar Chalamila,
Mchungaji Msigwa alisema kuwa lengo la kugawa kipindi hiki ni kuwaunga mkono
Waislamu katika mfungo wa Ramadhani na kuwakumbuka wale wote wanaoishi
katika mazingira magumu.
Mchungaji Msigwa alisema
ni jukumu la wadau kuweza kuwasaidia wale wote bila kujali itikadi za vyama kwa
kuwa binadamu wote ni wamoja kwa sasa.
Mchungaji Msigwa
alikabidhi tambi katoni zaidi ya katoni 50, katoni 40 za mafuta ya kupikia,
kilo 250 za unga wa ngano na sukari kilo 750 vyote vikiwa na jumla ya thamani
zaidi ya shilingi milioni 1.5.
Alisema ataendelea kutoa
msaada kwa vituo vingine vya watoto yatima na wasiojiweza katika kipindi hiki
cha mfungo wa Ramadhan.
Akishukuru kwa msaada
huo Kwa niaba ya chuo cha Kitanzani Islamic Center chenye jumla ya wanafunzi 120
ambao wanachukua mafunzo ya dini ya kiislamu Kaimu Shekhe Mkuu wa Mkoa Iringa,
Abubakar Chalamila alisema ni jambo la kujivunia kuwa na mbunge asiyechagua
itikadi za dini na mbunge ni akichaguliwa anakuwa wa watu wote bila kubagua
watu wake.
“Namshukuru sana Msigwa
kwa kuweza kutoa msaada huu na utafikishwa kwa wale wote waliolengwa
kupewa na hasa wale wasiojiweza ndio watafaidika na msaada huu wa mbunge wa
iringa mjini.” Alisema |Chalamila
Chalamila aliwataka
wadau wengine kuwakumbuka watu wasiojiweza na wanaoishi katika mazingira magumu
mara kwa mara kwa kuwa ni thawabu kubwa kuweza kuwasaidia.
No comments:
Post a Comment