Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu
mchimati@gmail.com au Tupigie n amba +255767869133/ +255-713-869133
Ni kama ajabu, lakini ndiyo hivyo baada ya jezi
yenye namba 10 aliyokabidhiwa staa huyo kuuzwa kama njugu ndani ya saa
48 tu tangu alipotambulishwa rasmi Jumanne iliyopita kuwa ni mchezaji wa
Real Madrid.
REAL Madrid imepiga bao. Imetoa pauni 63 milioni
kumnasa James Rodriguez na hata kabla hajaanza kucheza mechi yoyote
kuleta mataji klabuni hapo, pesa zao zimeanza kurudi.
Ni kama ajabu, lakini ndiyo hivyo baada ya jezi
yenye namba 10 aliyokabidhiwa staa huyo kuuzwa kama njugu ndani ya saa
48 tu tangu alipotambulishwa rasmi Jumanne iliyopita kuwa ni mchezaji wa
Real Madrid.
Ripoti zinabainisha kwamba Real Madrid hadi sasa
tayari imesharudisha kiasi cha pauni 21 milioni baada ya mauzo ya jezi
345,000 za Rodriguez ndani ya saa 48 tu.
Mashabiki wa timu hiyo wameonekana kupagawa na
usajili wa Rodriguez, ambaye amepewa jezi iliyokuwa ikivaliwa na Mesut
Ozil (kabla hajabadili na kuvaa namba 11) na mwaka jana kutimkia
Arsenal.
Kwa mujibu wa gazeti moja la michezo la Hispania,
kampuni ya wataalamu wa masoko ya kibiashara michezoni ilifanya hesabu
na kugundua kwamba jezi hizo 345,000 zilizouzwa kwa saa 48 ni sawa na
mauzo ya jezi 7,188 kwa saa. Hii ni rekodi.
Real Madrid haijawahi kusumbuka juu ya mauzo ya
jezi za mastaa wao wanaowasajili kwa pesa nyingi, lakini nyota huyo
aliyetamba kwenye Kombe la Dunia nchini Brazil mauzo ya jezi zake
zimeweka rekodi.
Kwenye utambulisho wake uliofanyika uwanjani
Bernabeu Jumanne iliyopita zaidi ya mashabiki 44,000 walijitokeza
kumshangilia mchezaji huyo huku wengine 900 tayari walionekana kuvaa
jezi za mchezaji wao huyo mpya.
Kwa mauzo hayo ya siku mbili tu ya jezi za
Rodriguez, tayari Real Madrid imebakiza pauni 3 milioni tu kurudisha
pesa walizomsajili kiungo Toni Kroos, aliyejiunga na timu hiyo kwa pauni
24 milioni kutoka Bayern Munich.
No comments:
Post a Comment