Ujumbe kutoka Bill & Melinda Gates Foundation umefanya ziara
Tanzania na kuitembelea pia TFDA kwa lengo la kujionea utekelezaji wa
miradi mbalimbali ya afya wanayoifadhili Tanzania.
Ujumbe
huo unaoongozwa na Mkurugenzi katika Mfuko huo Bw. Michael Poole,
umesifu maendeleo ya Mradi wa ADDO na Uwianisho wa mifumo ya udhibiti wa
dawa kwa nchi za Afrika Mashariki, miradi ambayo TFDA imekuwa
ikisimamia utekelezaji wa ADDO hadi mwaka 2012 na kushiriki Uwianisho wa
mifumo ya udhibiti wa dawa katika Jumuiya ya Afrika Mashariki toka
mwaka 2012 hadi sasa.
Hivi
sasa ADDO inasimamiwa na Baraza la Famasi kufuatia Sheria ya Famasi ya
mwaka 2011.Wenyeji wa ujumbe huu ni Shirika la Menejimenti ya Sayansi ya
Afya (MSH) ambao ni wadau wakuu wa mradi wa mpango wa ADDO nchini.
Picha ya kikao cha ueasilishaji wa taarifa za maendeleo ya miradi inayofadhiliwa na Mfuko huo
Picha ya pamoja ya ujumbe kutoka Mfuko wa Bill & Mellinda Gates,
Maafisa wa TFDA, MSH na Baraza la Famasi mara baada ya ziara ya TFDA.
Picha ya Kaimu Murugenzi Mkuu TFDA, Dkt. S.S Ngendabanka, akibadilishana
mawazo na Mkurugenzi wa Mfuko wa Bill & Mellinda Gates Bw. Michael
Poole katika viwanja vya TFDA
No comments:
Post a Comment