WATU
wanane wakiwemo Madaktari wa Chuo Kikuu cha Madaktari cha International
Medical and Technological University (IMTU), wanashikiliwa na Polisi
kwa tuhuma za kuhusika la utupaji viungo vya binadamu jalalani.
Polisi imesema mifuko ipatayo 85 yenye vichwa, miguu, mikono, moyo, mapafu, vifua na mifupa ya aina mbalimbali ya binadamu, ilikutwa juzi jioni katika maeneo ya bonde la Mbweni Mpiji, eneo la Bunju jijini Dar es Salaam.
Kamanda wa Polisi, Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova alisema baada ya uchunguzi, iligundulika viungo hivyo kwa mara ya mwisho vilikuwa katika maabara ya chuo kikuu hicho ambacho pia hufanya mafunzo kwa vitendo.
“Baada ya kuwahoji walikubali kuhusika na utupaji wa viungo hivyo na kuwakamata kwa ajili ya uchunguzi zaidi kujua kwa nini walivitupa kwa wingi kiasi hicho kwa wakati mmoja na siyo kuvihifadhi au kuharibu ikiwa walivitumia kwa ajili ya mafunzo,” alisema Kova.
Alisema katika eneo hilo, pia vilikutwa vifaa vinavyotumika hospitalini kama vile mipira ya kuvaa mikononi, mifuko miwili iliyotumika, nguo maalumu zipatazo 20 na karatasi mbili zenye maswali ya kujibu.
Kova alisema siku hiyo ya tukio, wananchi wasiopungua 1,000 walifika katika eneo hilo na hakuna aliyefahamu vilikotoka ndipo walitoa taarifa Polisi.
Polisi walivichukua viungo hivyo na kupeleka katika Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa uchunguzi, uliofanywa na jopo la wapelelezi chini ya Mkuu wa Upelelezi, Kanda Maalumu, Japhari Mohamed.
Uchunguzi huo ulifanywa kwa kusaidiana na Daktari wa Jeshi la Polisi, anayehusika kuchunguza miili ya binadamu; akishirikiana na madaktari wengine wa Muhimbili.
Jopo kuchunguza
Katika kuhakikisha majibu yote yanajibiwa ikiwa ni pamoja na kujua idadi kamili ya watu wenye viungo hivyo, Kova alisema imeundwa timu ya wataalamu ya watu saba ikihusisha Mkemia Mkuu wa Serikali, kupata taarifa sahihi za kipolisi.
Kwa kutumia jopo hilo, kwa mujibu wa Kamanda, itabainika viungo hivyo ni vya muda gani na zilitumika kemikali gani kuvikausha. Jopo litabaini pia kama ipo sheria na ni ipi inavunjwa. Inalenga kubaini pia kama upo uzembe katika kulinda viungo vya binadamu na vinapatikanaje kwa ajili ya mazoezi.
Hakuna vifo vya halaiki
Kamanda Kova alitaka wananchi kuwa na subira wakati uchunguzi ukiendelea na kusisitiza, hakuna vifo vya watu wengi vilivyotokea kwa wakati mmoja isipokuwa ni miili ya muda mrefu iliyotumika kwa mafunzo.
“Serikali inashughulikia suala hili. Baada ya upembuzi yakinifu, tutatoa taarifa na hatua kali zitachukuliwa kwa wote waliohusika katika sakata hili la kutupa miili ya binadamu hawa,” alisema.
Viungo vilitupwaje?
Akizungumzia jinsi viu ngo hivyo vilivyofika maeneo hayo, Kova alisema taarifa za kipolisi zinasema alifika mtu mmoja maeneo hayo akiwa na kiongozi mmoja wa chuo hicho na kumwaga mifuko hiyo kisha kuondoka.
Kuhusu gari linalodaiwa lilifika maeneo hayo siku ya tukio, alisema halihusiki na ubebaji wa viungo hivyo, isipokuwa lilikuwa limebeba mabaki ya kuku ikiwemo utumbo ,vichwa na vinginevyo kutoka Kampuni ya Interchick vikitoa harufu kali.
Kova alisema baada ya kufika maeneo hayo na wananchi kusikia harufu, walianza kukimbiza gari hilo kwa kutumia pikipiki. Dereva wa gari hilo alipoona hivyo, alikimbilia Kituo cha Polisi na baada ya kuchunguza na kuona mabaki ya kuku, Polisi walimsindikiza na kutupa mabaki hayo.
Wizara yazungumza
Akizungumzia suala hilo, Msemaji wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Nsachris Mwamwaja aliahidi kuzungumzia kwa undani suala hilo leo.
Mwamwaja ambaye alisema utupaji huo wa miili si mzuri na sahihi kiafya, aliahidi kuzungumzia suala hilo kutokana na kuulizwa na mwandishi utaratibu na mwongozo wa utunzaji, uondoshaji wa miili au viungo vya mwili vinavyotumiwa katika vyuo vikuu mbalimbali kwa ajili ya mafunzo kwa vitendo.
Kamata kamata Waandishi wa gazeti hili walishuhudia polisi wakiwachukua baadhi ya viongozi wa IMTU na kuondoka nao. Walishuhudia msafara wa magari zaidi ya matano, yakiongozwa na Mkuu wa Upelelezi wa Wilaya ya Kipolisi wa Kinondoni .
Waliondoka na viongozi hao hadi Kituo cha Polisi cha Oysterbay. Hata hivyo, haikufahamika mara moja ni viongozi gani waliochukuliwa kulingana na nyadhifa na majina yao.
Madai yatolewa Kwa mujibu wa taarifa kutoka chuo hicho, miili hiyo iliyotumiwa Semesta ya Kwanza, Machi mwaka huu, ilitakiwa kufanyiwa utaratibu wa kuondolewa hospitalini hapo.
Ingawa haijafahamika ni utaratibu gani unatumika kuondoa miili inayotumiwa kwa mazoezi, taarifa kutoka chuoni zinadai kifaa maalumu cha kuteketeza miili hiyo kiliharibika.
Mashuhuda
Mwandishi wa gazeti aliyefika eneo la tukio, alishuhudia gari hilo lenye namba za usajili T 166 CAF, maarufu kama ‘Kirikuu’, ambalo dereva wake alinusurika kuuawa na wananchi waliokuwa wakimtuhumu kutupa vifurushi hivyo vyenye viungo vya binadamu.
Inadaiwa watu wanaojishughulisha na upasuaji kokoto katika eneo hilo la Mpiji, ndiyo waligundua baada ya kwenda katika jalala hilo kwa madhumuni ya kuokota mifuko ya plastiki kwa ajili ya matumizi yao.
“Sisi tumekuja kuokota mifuko kwa ajili ya kwenda kutumia kuezeka katika nyumba zetu cha kushangaza na kushtusha ni baada ya kufungua mfuko, na katika kumwaga taka zilizo ndani, bila ya kutegemea kikadondoka kichwa cha mtu na mguu uliokatwa huku ukiwa umechunwa ngozi,” alisema mmoja wa mashuhuda

No comments:
Post a Comment