Mratibu wa Tamasha la
Nacte Inter College Tanzania 2014/15- (BONANZA). Bi. Magreth
Kilawe(kulia), akifafanua jambo kuhusiana na Michezo ya Vyuo Vya Elimu
ya Kati, katika ngazi ya Cheti na Stashahada, ambayo inaanza kufanyika
katika Vyuo Mbalimbali hapa Nchini, katika hafla iliyofanyika kwenye
Ukumbi wa Idara Habari Maelezo, Dar es Salaam,Leo, kushoto ni Mkurugenzi
wa Kampuni na Mwenyekiti wa Kamati ya NACTE INTER COLLEGE TANZANIA, Mh,
Mpalule Shaaban,
(Picha Zote Kwa Hissani ya Miss Demokrasia Tanzania).
Waandaaji wa Tamasha la NACTE INTER COLLEGE TANZANIA 2014/2015, kutoka Kulia ni Mwakilishi wa Wakuu wa Vyuo vya NACTE TANZANIA, Mwl. Kasilima, Mwenyekiti wa Kamati Mh.Mpalule Shaaban, Mratibu wa Tamasha, Bi, Magreth Kilawe, Afisa Mahusiano wa Miss Demokrasia Tanzania, Bi, Rosina Mchomvu na Bi, Jane Charles kutoka Ikondolelo Hoteli Lodge, wadhamini wa Vikao vya Maandalizi.
Mwenyekiti wa Kamati Mh.Mpalule Shaaban, Mratibu wa Tamasha, Bi, Magreth Kilawe, Afisa Mahusiano wa Miss Demokrasia Tanzania, Bi, Rosina Mchomvu
Mwenyekiti wa Kamati Mh.Mpalule Shaaban, Mratibu wa Tamasha, Bi, Magreth Kilawe, Afisa Mahusiano wa Miss Demokrasia Tanzania.
Mwenyekiti wa Kamati Mh.Mpalule Shaaban, Mratibu wa Tamasha, Bi, Magreth Kilawe, Afisa Mahusiano wa Miss Demokrasia Tanzania,
Mwenyekiti wa Kamati Mh.Mpalule Shaaban, Mratibu wa Tamasha, Bi, Magreth Kilawe, Afisa Mahusiano wa Miss Demokrasia Tanzania.
Baadhi ya Waandishi wa Habari wa vyombo mbali wakifuatilia kwa makini Mazungumzo wakati wa kuelezea Tamasha la NACTE INTER COLLEGE TANZANIA.
Mwakilishi wa wakuu wa vyuo, Mwl Kasilima kutoka kushoto, Mwenyekiti wa Kamati Mh.Mpalule Shaaban,Mwakilishi wa Serikali za Wanafunzi na Mshauri wa Chuo cha C.B.E-Dar es salaam, Mr. Stephano, Mratibu wa Tamasha, Bi, Magreth Kilawe.
kutoka kushoto ni Mwakilishi wa wakuu wa vyuo, Mwl Kasilima, Mwenyekiti wa Kamati Mh.Mpalule Shaaban,Mwakilishi wa Serikali za Wanafunzi na Mshauri wa Chuo cha C.B.E-Dar es salaam, Mr. Stephano, Mratibu wa Tamasha, Bi, Magreth Kilawe.
Mratibu wa Tamasha, Bi, Magreth Kilawe,(kati)akifafanua jambo, wengine Mdhamini mdogo wa Tamasha kutoka Mlonge Moringa, wanaojiusisha na masuala ya Dawa na Vipodozi kuoka mlonge, Mwakilishi wa Serikali za Wanafunzi na Mshauri wa Chuo cha C.B.E-Dar es salaam, Mr. Stephano,wa pili kulia ni Afisa Uhusiano wa Miss Demokrasia Tanzania, Bi. Rosina Mchomvu, na Mwakilishi wa IKONDOLELO LODGE, Mdhamini wa Vikao vya Maandalizi, Bi. Janet Charles
Mratibu wa Tamasha, Bi, Magreth Kilawe,(kulia)wengine ni Mdhamini mdogo wa Tamasha kutoka Mlonge Moringa(kushoto), wanaojiusisha na masuala ya Dawa na Vipodozi kuoka mlonge, Mwakilishi wa Serikali za Wanafunzi na Mshauri wa Chuo cha C.B.E-Dar es salaam, Mr. Stephano
Mwenyekiti wa Kamati ya NACTE INTER COLLEGE TANZANIA 2014/2015, Mh.
Mpalule Shaaban, akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari, Idara
Habari Maelezo, kuhusiana na Tamasha la Vyuo vya Elimu ya Kati na
Vilivyopata Usajili wa NACTE, wengine ni (wa pili kulia)Mratibu wa Tamasha, Bi, Magreth Kilawe,(kati,Mdhamini mdogo wa Tamasha kutoka Mlonge Moringa, (wa tatu kushoto), wanaojiusisha na masuala ya Dawa na Vipodozi kuoka mlonge, (kati ni Mwakilishi wa Serikali za Wanafunzi na Mshauri wa Chuo cha C.B.E-Dar es salaam, Mr. Stephano na Afisa Uhusiano wa Miss Demokrasia Tanzania, Bi, Rosina Mchomvu.
Wandishi wakifuatilia.
Bidhaa mbalimbalia zitokano za zao la MLONGE, wakati wa Hafla ya Waandishi wa Habari, Waandaaji na Wadhamini.
Viongozi wa Tamasha la NACTE TANZANIA.
Viongozi
Mratibu wa Tamasha, Bi, Magreth Kilawe,(kati)akiwa na baadhi ya Wanakati na wawakilishi wa Vyuo, na Mdhanini Mdogo.
--------------------------------------------------
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
PRESS RELEASE
NACTE
INTER - COLLEGE TANZANIA BONANZA 2014/15.
(BALOZI
WA DEMOKRASIA TANZANIA).
24/7/2014
HABARI za wakati huu,
Waandishi wa habari wote, wakuu wa vyuo na viongozi wa Serikali
Waandishi wa habari wote, wakuu wa vyuo na viongozi wa Serikali
za wanafunzi wa vyuo shiriki, wadhamini, Karibuni
sana.
Leo ni siku rasmi, ya kutangaza
kuanza kwa mchakato mzima
wa maandalizi ya mashindano ya NACTE Inter-College
Tanzania Bonanza 2014/15, ambayo kwa mara ya kwanza yataanza kuonesha sura na
muonekano mpya katika Sekta ya Elimu kwa ngazi ya Vyuo vya Kati.
Bonanza hili limepangwa kufanyika
21-23/11/2014 katika viwanja
vilivyopendekezwa ikiwa ni pamoja na The Mwalimu
Nyerere Memoria Academy,(Kigamboni) Chuo Kikuu Dar es Salaam, Leaders Club, TCC
Sigara (Chang’ombe, na viwanja vya Shule ya Sekondari Kibaha Katika michezo
mbali mbali .
Ndugu wandishi, tamasha hili lipewa kibali na baraza
la elimu ya ufundi yaani NACTE katika barua yao ya tarehe 21/6/2014 yenye kumb
No. NACTE/EB/64/650/Vol.1/2 ambayo
inairuhusu kampuni ya Miss Demokrasia Tanzania, kuandaa na kuwa mwenyeji wa
Tamasha la NACTE Inter College Tanzania.
Nichukue fursa hii kuishukuru Serikali kwa kukubali
kuipa heshima kubwa kampuni ya Miss Demokrasia Tanzania, ubavu wa kuandaa
tamasha hili, lakini pia tunaiomba Serikali kuhamasisha wadau kujitokeza
kusaidia vifaa vya michezo hii.
kwa kushirikiana na vyombo vya habari hapa nchini na vyuo husika,
Wadhamini ambao hao ni wadau namba moja, wawezeshaji tutaifanaya kwa ustadi na kwa makini mkubwa
ili mwaka ujao kuwe na msisimko zaidi,
ikumbukwe kuwa michezo hii inafanyika kwa mara ya kwanza hapa
Tanzania. Itakuwa ni fursa kwa wanafunzi wa vyuo vya kati, kwa nafasi zao
kuendeleza vipaji walivyonavyo, kwa kuwa,
kwa muda mrefu hawajapata nafasi kama
hii, ya kushiriki katika michezo pindi
wanapoingia kwenye vyuo, baada ya masomo
ya Elimu za Sekondari.
Ndugu waandishi, Michezo, kama
tunavyofahamu ndiyo pekee inayoweza kutoa fursa kwa vijana, kupata afya nzuri, ajira katika michezo,
pamoja na nafasi ya kuitangaza Tanzania,
kupitia Michezo vijana upata fursa ya
kusikilizwa na kufikisha mawazo yao, na mambo mbalimbali yanayohusu afya na
maendeleo yao ikiwemo Ujasiriamali, Elimu ya UKIMWI na mengine mengi yakiwemo
kutambua nafasi ya kijana katika kutunza na kulinda amani ya Nchi yetu.
Pamoja na kuwa na nchi yenye amani; michezo
pia utoa fursa ya vijana kujiendeleza kiujasiriamali, lakini pia kwa kupitia tamasha hili inaweza
kuwa fursa ya makampuni, wahisani, wadau, kukamilisha ndoto zao, katika kuongeza
wigo wa ajira kwa vijana wanaohitimu vyuo vya kati.
tumieni kalamu zenu, Mic, Kamera, kuhamasisha Michezo
hii na Wadau kujitokeza kusaidia michezo hii ya vyuo vilivyo pata usajili wa
NACTE.
wito unatolewa kwa vyuo, kuthibitisha
ushiriki wao mapema, kabla ya tarehe 15/8/2014, Michezo hii ni kwa vyuo vyote vya
NACTE Tanzania, baada ya Dar es salaam, itafuata Mikoa ya Mwanza, Arusha,
Mbeya, Dodoma na Zanzibar Fomu zinapatikana kwenye Tovuti,
Kampuni ya Miss Demokrasia Tanzania, ilianzishwa
Mwaka 2009, na kupata Usajili wa kudumu wa Makampuni unaotambuliwa Kisheria wa
Act, 2002 No. 74413 mwaka 2010, na TIN No: 109-267-554. Kampuni hii ambayo kwa
ujumla kama lilivyo jina lake, (Miss Demokrasia Tanzania) ina malengo mengi, ikiwa
na pamoja na kusaidia jamii hususani vijana wa kike, ambao muda mwingi wamekuwa
wakishindwa kufikia malengo kutokana na ukosefu wa miundo mbinu ya kujikomboa
kielimu, Utamaduni na Michezo, Ajira,
kwani wengi wao wameoonewa na kunyimwa haki zao.
kampuni hii inalinda na kutetea haki
za watu wote ikiwa ni pamoja na kuwapa changamoto Viongozi mbali mbali wa
serekali na Taasisi binafsi dhidi ya utendaji wao wa kazi na majukumu ili
kuongeza na kuboresha ufanisi wao wa kazi kwa wananchi, imejikita sana kwenye
masuala ya Intertainment Michezo, Maonesho, Burudani, Mikutano, Mijadala
(Debate), Elimu kwa Jamii, na Urembo (Modal) kwa namna ya kipekee.
Mwisho: kabisa
nirudie tena kuishukuru Serikali na Uongozi wa NACTE kwa kuweka na kukubali
mpango huu wa Michezo kwenye vyuo vya kati. Tutumie nafasi hii, kuwakaribisha
wahisani na Wadhamini wote, kushiriki kikamili na kwa namna yoyote ile ili
kufanikisha Tamasha hili la NACTE – INTER – COLLEGE - TANZANIA – 2014 / 2015.
Niwashukuru wadhamini walioanza
kujitokeza, IKONDOLELO HOTELI Lodge wanaopatikana Kibamba CCM, MLONGE MORINGA,
na Tone on line Radio T-z. Baada ya kusema hayo. Asanteni Wote kwa kunisikiliza. niwape nafasi
wawakilishi wa Vyuo, na wadhamini waseme japo waliyo nayo…
Magreth Kilawe
Rosina
Mchomvu
Afisa Masoko Afisa
Habari
Kwa Mawasiliano Zaidi:
Miss Demokrasia Tanzania and Entertainment C.o LTD.
Plot No.
S.L.P 8017, Dar Es Salaam,
Simu: +255-767-869-133
+255-765-056-399
Email: missdemokrasiatanzania@yahoo.com,
Blogs:
www.missdemokrasia.blogspot.com,
Website: http://www.missdemocrasiatz.com/
No comments:
Post a Comment