Katibu
wa NEC Itikadi na Uenezi CCM Taifa Nape Nnauye amesema Chama Cha
Mapinduzi hakimzuii mwanachama yeyote kutangaza nia ya kugombea Uongozi
katika muhula unaofuata isipokuwa Chama kimezuia kampeni za mapema kwani
ndio chanzo cha makundi ndani ya Chama akizungumza kwenye kipindi cha
Baragumu kinachorushwa na Channel 10.
Nape
alisema taratibu za kugombea Uongozi ndani ya chama zipo na kuna Kanuni
mbili, moja ni ya Kanuni za Viongozi na Maadili na pili Kanuni
zinazosimamia Uchaguzi ndani ya CCM, akinukuu kutoka kwenye kitabu cha
Kanuni za Viongozi na Maadili ,Nape alisema "Wanachama wenye nia ya
kugombea nafasi ya uongozi katika muhula unaofuata anaweza kutangaza nia
ya kugombea lakini haruhusiwi kufanya kampeni kabla ya muda".
Akizungumzia juu ya adhabu wanazopewa waliokiuka alisema adhabu hizi
zina shabaha ya kuwasaidia wanachama na Viongozi kujirekebisha.Nape pia
alizungumzia suala zima la upatikanaji wa Katiba Mpya,alisema CCM
imeshikamana sana kiasi cha kuwachanganya Wapinzani, aliendelea kwa
kusema Kanuni,Sheria zinazotumika ni makubaliano ya wote.(Wapinzani
walishiriki katika kamati kutengeneza kanuni na sheria na zikapitishwa
Bungeni wakiwemo na Rais akasaini).
Chanzo: kamerayangublog.com
No comments:
Post a Comment