Mgeni
rasmi Mkuu wa wilaya ya Kilolo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa,
Gerald Guninita akiweka ngao ya jadi katika sehemu inayotarajiwa
kujengwa Mnara wa Mashujaa wa Jeshi la Mkwawa waliopigana vita dhidi ya
dhuluma za Wajerumani, Mnara huo upo karibu na walipozikwa askari wa
kijerumani 300 wakati wa vita na chifu wa wahehe Chifu Mkwawa mnamo
mwaka 1891 wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Mashujaa yaliofanyika kimkoa
katika Kijiji cha Lugalo wilayani Kilolo mkoani Iringa.
Askari
wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi Tanzania (JWTZ) wakipita kwa gwaride la
heshima katika maadhimisho ya siku ya mashujaa yaliofanyika kimkoa
katika Kijiji cha Lugalo wilayani Kilolo mkani Iringa leo.
Mkuu wa wilaya ya Kilolo Gerald Guninita(Kushoto) akiwa pamoja na mwenyekit wa Halmashauri ya wilaya hiyo
Joseph Muhumba wakitoa heshima wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Mashujaa yaliofanyika kimkoa katika Kijiji cha Lugalo wilayani Kilolo.
Joseph Muhumba wakitoa heshima wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Mashujaa yaliofanyika kimkoa katika Kijiji cha Lugalo wilayani Kilolo.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya,Pudenciana Kisaka (mwenye pinki) sambamba na wakuu wa wilaya ya Mufindi na Iringa wakitoa heshima wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Mashujaa yaliofanyika kimkoa katika Kijiji cha Lugalo wilayani Kilolo.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Iringa ACP, Ramadhani Mungi akiweka silaha ya jadi
(mkuki) kwenye mnara wa mfano wa mashujaa. Mnara wa mashujaa wa askari
wa Chifu Mkwawa utarajia kujengwa mahali hapo karibu na mnara wa
wajerumani 300 waliozikwa katika Kijiji cha Lugalo wilayani Kilolo, Mkoa
wa Iringa.
Baadhi ya wananchi waliohudhuria maadhimisho hayo. (Picha zote na Denis Mlowe)
No comments:
Post a Comment