Naibu Katibu Mkuu wa
Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Ngosi Mwihava (kushoto) akifungua rasmi
mafunzo
yanayowakutanisha wataalamu kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Ofisi ya
Makamu wa Rais – Mazingira na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam yanayoendelea mjini
Morogoro. Aliyekaa upande wa kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Usimamizi wa
Mazingira kutoka Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Gidion Kasege.
Mmoja wa
wawezeshaji Profesa Pius Yanda kutoka Kituo cha Taaluma ya Mabadiliko ya
Tabianchi kilichopo chini ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam akiwasilisha mada
wakati wa mafunzo hayo
Baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo wakifuatilia kwa
makini mada zilizokuwa zinawasilishwa na wawezeshaji kwa nyakati tofauti
tofauti
Mkuu wa Kitengo cha
Usimamizi wa Mazingira Mhandisi Gidion
Kasege (kulia) na Afisa Mazingira
Mkuu na Mratibu wa Mradi wa EMA-ISP Bw. Theodore Silinge kutoka Wizara ya
Nishati na Madini wakifuatilia kwa makini mada zilizokuwa zinawasilishwa
Afisa Mazingira Mkuu na
Mratibu wa Mradi wa EMA-ISP kutoka Wizara ya Nishati na Madini Bw. Theodore
Silinge akisisitiza jambo wakati wa mafunzo hayo
Mtaalamu kutoka Idara
ya Nishati iliyopo chini ya Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Nyaso Makwaya
akisisitiza jambo wakati alipokuwa akiwasilisha
mada kuhusiana na mikakati ya Wizara katika kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi.
Mkuu wa Kitengo cha
Usimamizi wa Mazingira kutoka Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Gidion Kasege
(kulia) akizungumza kabla ya kumkaribisha Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya
Nishati na Madini Mhandisi Ngosi Mwihava
(aliyekaa kulia kwake) ambaye alikuwa ni mgeni rasmi kwenye ufunguzi wa mafunzo
yanayowakutanisha wataalamu kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Ofisi ya
Makamu wa Rais – Mazingira na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam yanayoendelea mjini
Morogoro.
Washiriki wa mafunzo ya Mabadiliko ya Tabianchi yanayoendelea mjini Morogoro wakiwa katika
picha ya pamoja na Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Ngosi Mwihava (wa nne
kutoka kushoto waliosimama mstari wa mbele) mara baada ya ufunguzi wa mafunzo
hayo
No comments:
Post a Comment